Beki wa Simba, Komabi Keita (chini) akislid kuokoa moja ya hatari (juu) ni mshambuliaji wa Libolo, akikwepa kwanja. Katika mchezo huo Libolo ya Angola, imeibuka na ushindi wa bao 1-0, bao lililofungwa na Joao Martins, katika dakika ya 24.
Shaban Kapombe (kulia) akichuana kuwania mpira na mchezaji wa Libolo.
Keita, akiokoa moja ya hatari katikati ya washambuliaji wa Libolo.
Beki wa Simba, Komabi Keita (chini) akislid kuokoa mpira.
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Liewig (kulia) akizungumza jambo na msaidizi wake, Jamhuri.
Winga wa Libolo, akijiandaa kupiga krosi, huku beki wa Simba Juma Nyoso, akijiandaa kumkabili.
Wachezaji wa Libolo, wakishangilia baada ya kutupia bao lao katika dakika ya 24, kipindi cha kwanza.
Sehemu ya Mashabiki wa Libolo,
Kocha wa Simba, akiwaelekeza jambo wasaidizi wake wakati mchezo ukiendelea.
Kikosi cha kwanza cha Libolo.
Kikosi cha kwanza cha Simba.
Kocha wa Simba, Patrick Liewig, akiwa ameduaa baada ya mpira kumalizika.
******************************
BAO pekee lililofungwa
na Joao Martins katika dakika ya 24, limeifanya CRD Libolo ya Angola kuibuka na
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika
jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Martins alifunga bao
hilo kwa kichwa akiunganisha krosi safi ya Carlos Almeida kutoka wingi ya
kulia. Almeida alipiga krosi hiyo mbele ya mabeki Shomari Kapombe na Mussa
Mudde.
Matokeo hayo yanaifanya
Simba kutakiwa kupambana kufa na kupona katika mchezo wa marudiano utakaochezwa
wiki mbili zijazo huko nchini Angola.
Simba inatakiwa kushinda si chini ya bao
1-0 au idadi yoyote ya ushindi wenye kulingana na 1-0.
Hadi kipindi cha kwanza
kinamalizika, timu hizo zilikuwa zikishambuliana kwa zamu lakini Libolo
ilionekana kuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira.
Katika kipindi cha
kwanza, Libolo ilizima mashambulizi mengi ya Simba huku sehemu yake ya kiungo ikionekana
kuwa imara kuliko Wekundu wa Msimbazi.
Kipindi cha pili timu
zote zilikianza kwa kushambuliana kwa zamu lakini kama ilivyokuwa kipindi cha
kwanza, lakini mipango mingi ya Simba katika idara ya kiungo haikufua dafu.
Viungo wa Simba, Amri
Kiemba, Mwinyi Kazimoto na Mrisho Ngassa walijitahidi kuipenya ngome ya Libolo lakini
viungo wa timu hiyo Manuel Lopes, Sidnei Mariano na Dorivaldo Dias walikuwa
imara kuokoa hatari zote.
Katika kipindi cha pili
Simba ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Mussa Mudde (dk 53), Haruna Chanongo (dk 66)
na Haruna Moshi ‘Boban’ (dk 84) na nafasi zao kuchukuliwa na Amir Maftah, Ramadhan
Singano ‘Messi’ na Salum Kinje.
Kwa upande wao Libolo,
waliwatoa Joao Martins (dk 72), Dario Cardoso (dk 82) na Maieco Antonio (dk 76)
na nafasi zao kuchukuliwa na Andres Madrid, Nuno Silva na Henry Camara.
Hata hivyo, mabadiliko
hayo hayakuweza kubadili matokeo ya mchezo huo ulioudhuriwa na mashabiki wengi
kiasi.
Dakika ya 83, Boban
alimpiga kiwiko beki wa Libolo, Pedro Ribeiro lakini mwamuzi hakuchukua hatua
yoyote kwani hakumuona Boban akitenda kosa hilo.
Dakika ya 94, Libolo
ilitawala mchezo kwa kugongeana pasi 25 ndani ya sekunde 50.
No comments:
Post a Comment