Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linazitakia kila
la kheri timu za Azam, Jamhuri na Simba ambazo zinaiwakilisha Tanzania katika
michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.
Azam inacheza na Al Nasir Juba ya Sudan Kusini katika mchezo
wa Kombe la Shirikisho utakaofanyika Jumamosi (Februari 16 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Nayo Jamhuri ya Zanzibar kesho itacheza na St. Georges ya
Ethiopia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaofanyika Uwanja wa
Gombani kisiwani Pemba. Simba itacheza na Recreativo do Libolo ya Angola
keshokutwa (Februari 17 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment