Mbunge wa Jimbo la Chambani kupitia Chama cha CUF, Salim Hemed Khamis, aliyeanguka ghafla jana wakati akiwa katika Kikao cha Bunge katika Ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam, amefariki dunia leo alipkuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu. Habari zaidi za taratibu za shughuli za maziko zitawajia kadri zitakavyopatikana.
Mbunge huyo akipata huduma ya kwanza jana baada ya kuanguka ghafla, wakati akihudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ambapo alikimbizwa Hospitali ya Taifa na kulazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi ICU ambako hadi umauti unamkuta alikuwa amelazwa.


No comments:
Post a Comment