Habari za Punde

*NAIBU MEYA MANISPAA YA KINONDONI AKUTANA NA KAMATI YA MAANDALIZI YA MISS UTALII TANZANIA TAIFA 2013

Rais wa Miss Utalii Tanzania, Erasto Chipungahero (kushoto) Kaimu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Songoro na Adam Chipungahero wakiwa katika mazungumzo katika Ofisi ya Meya huyo, jana.
Kamati ya Maandalizi ya Miss Utalii Tanzania, ikiongozwa na Rais wa Mashindano hayo, Erasto G. Chipungahelo, Jana ilipiga hodi katika ofisi ya Meya wa Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Katika mazungumzo yao, Chipugahelo, alimshukuru Naibu Mstahiki Meya, kwa  mapokezi na ushirikiano wanaopata kutoka kwa Manispaa hiyo ambapo warembo wapo kambini katika Hoteli ya Ikondolelo Lodge iliyopo Kibamba  Manispaa ya Kinondoni. 

Aidha Chipungahero, alimuhakikishia Naibu Meya, Kuwa Miss Utalii Tanzania Imejipanga kutangaza Utalii, Utamaduni na Mianya ya uwekezaji Manispaa ya Kinondoni kitaifa na Kimataifa ili hatimaye Kinondoni iwe kati ya Wilaya zenye sura ya jiji la Dar.

Akizungumza katika Kikao Hicho Naibu Mstahiki Meya, Aliwashukuru waandaaji wa Mashindano Hayo kwa Kuteuwa Manispaa ya Kinondoni kuwa makazi ya warembo wa Miss Utalii Tanzania Taifa 2012/13. 

''Hii ni Fulsa pekee kwa Manispaa yetu Kimataifa  lakini pia ni Fulsa kwa Manispaa ya Kinondoni kuuthibitishia Ulimwengu kuwa Tunavivutio vingi vya utalii ikiwa ni pamoja na mahoteli na maeneo ya kihistoria,  Fukwe za Bahari na visiwa vya kuvutia''. alisema Mstahiki

Chipungahero aliongozana na baadhi ya Viongozi wa Kamati hiyo ambao ni Adam Chipungahelo, Mratibu wa Matukio Miss Utalii Tanzania, Fredy Njeje, Meneja wa Masoko na mahusiano Miss Utalii Tanzania. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.