Habari za Punde

*MWANADADA HELEN JOSEPH KUWANIA UBINGWA WA IBF NA MARIANNA GULYAS

Bondia mwanadada, Helen Joseph, ambaye anaishi katika jiji la Accra, nchini Ghana akijishughulisha zaidi na kupigana ngumi, yuko mboni kupanda kilele cha mafanikio katika maisha yake ya ngumi. 

Hii ni fursa aliyokuwa akiisubiri kwa hamu kubwa katika maisha yake ya ngumi mwanadada huyu, Helen Joseph, anayetokea nchini Nigeria.
Mwaka jana alikutana na bondia Dahianna Santana, katika jiji la San Domingo, nchini Dominican Republic kugombea ubingwa wa dunia wa IBF katika uzito wa Unyonya (Fearherweight). 
Taabu na kashikashi zote alizozipata wakati wa patashika ile ya mwaka jana zimekuwa fundisho tosha kwa Helen, wakati anapojiandaa kukutana na Marianna Gulyas, kutoka nchini Hungary kugombea ubingwa wa IBF wa mabara katika uzito wa unyoya.
Mpambano huo, unaoandaliwa na kampuni maarufu ya kukuza ngumi ya GoldenMike Boxing Promotion Syndicate ya nchini Ghana, unategemewa kuwa wa patashika kutokana na mabondia wote wawili kuwa na ujuzi na makeke wawapo ulingoni. 
Madada hawa wanatarajia kupanda ulingoni Machi 30, katika uwanja wa michezo wa Accra na mpambano huu utarushwa moja kwa moja kupitia kituo cha luninga cha Super Sports.
Ni mapromota na mameneja wachache  ambao wanaweza kuwekeza kiasi kikubwa hivyo cha pesa katika mchezo wa ngumi, ambapo kampuni ya Golden Mike Boxing Promotions Syndicate ya nchini Ghana imewekeza katika kuinua kipaji cha mwana dada Helen Joseph.
Kwa upande wake Helen ambaye ni nadhifu, mtanashati na mwenye nidhamu ya hali ya juu, katika mchezo wa ngumi, akiheshimu mchezo huo kuwa kuamini kuwa ndio hasa unaomwendeshea maisha yake, ameahidi kutumia uwezo wake wote kuhakikisha kuwa taji hilo kubwa la ngumi linabaki barani Afrika na kulitumia kama ngazi ya kukutana tena na Dahianna Santana katika ubingwa wa dunia.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.