Habari za Punde

*ODINGA 'AKUBALI YAISHE, UHURU RAIS RASMI KENYA


Mahakama  ya Juu nchini Kenya leo, imetoa maamuzi ya kesi iliyofunguliwa na mpinzani wa Uhuru Kenyatta, Raila Odinga, kuhusu kupinga matokeo ya uchaguzi na hatimaye imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na Odinga ambaye awali alidai kuwa kura zilichakachuliwa na mashine za uchaguzi zilijaa kwikwi, ambapo kwa sasa uamuzi huo umesafisha njia kwa Uhuru Kenyatta kuingia Ikulu. Na sasa anatarajiwa kuapishwa wiki ijayo April 9, 2013.

Habari zimeingia sasa hivi zinasema aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Mhe Raila Odinga amekubali uamuzi wa mahakama kuu, kuashiria kwamba sasa mambo ni tambarare, na sio kama iivyohofiwa awali kuwa kutatokea vurugu kama za uchaguzi wa mwaka 2007.

“Ni uamuzi wa mahakama hii kwamba walalamikiwa wa tatu na wa nee walichaguliwa kwa haki”, alisema Jaji Mkuu wa Kenya Willy Mutunga, wakati wa kutoa uamuzi hu, akimaanisha Kenyatta na mgombea mwena na Naibu Rais William Ruto wameshinda kihalali.

Jaji Mkuu huyo alisema mahakama imetekeleza wajibu wake katika muda huo wa kihistoria. “Sasa ni juu ya Wakenya, viongozi wao, taasisi za kijamii, sekta binafsi na vyombo vya habari kutekeleza wajibu wao kuhakikisha umoja, amani, utaifa na maendeleo ya taifa vinahifadhiwa”, aliongezea.

Rais mteule wa Kenya huyo alimshinda mpinzani wake kwa asilimia 50.07 dhidi ya asilimia 43,28 za Odinga.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.