Habari za Punde

*SIMBA, KAGERA SUGAR KUKIPIGA KESHO LIGI YA VODACOM


Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania inaendelea kesho (Machi 27 mwaka huu) kwa mechi mbili ambapo bingwa mtetezi Simba atakuwa mgeni ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 3,000 unatarajiwa kushuhudia mechi yenye ushindi kutokana na uwezo wa wachezaji wa pande zote mbili.

Mechi nyingine itapigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam kati ya wenyeji Azam na Tanzania Prisons kutoka Mbeya.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.