Habari za Punde

*UZINDUZI WA SHINDANO LA REDD'S MISS TANZANIA 2013

Baadhi ya Warembo walioshirikishi Shindano la Redd’s Miss Tanzania 2012 wakicheza muziki wa Kwaito wakati wa tafrija maalum ya uzinduzi wa Mashindano ya Miss Tanzania 2013 iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana usiku. Kulia ni Redd’s Miss Tanzania 2012, Brigit Alfred.

 Redd's Miss Tanzania 2012, Brigit Alfred (katikati) akigonganisha glass na Mkurugeni wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambao ni Wadhamini wakuu wa Shindano la Miss Tanzania, Kushilla Thomas (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Lino International Agency waandaaji wa Miss Tanzania, Anko Hashim Lundenga, ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa mbio za kumsaka Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakati wa tafrija mchaparo a.k.a mkia wa jogoo (cocktail party), iliyofayika jana kwenye Ukumbi wa Maqee,uliopo Serena Hoteli,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency ya Jijini Dar es Salaam, ambao ndio waandaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga, akitoa hotuba ya ufunguzi, wa Shindano la kumsaka Malkia wa Tanzania 2013.

Hii ndio ilikuwa tatu bora ya Miss Tanzania 2012, Mshindi wa Taji la Redds Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred (katikati) akiwa pamoja na washindi wenzake, Eugene Fabian aliyetwaa nafasi ya pili (kulia) na Mshindi wa Tatu, Edda Sylvester.
 Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania, Mzee Ole Naiko (kulia) akizungumza na wanakamati ya Miss Tanzania na Miss Tanzania 2012.
 Redds Miss Tanzania 2012, Brigit Alfred akitoa hotuba ya ufunguzi, wa Shindano la kumsaka Malkia wa Tanzania 2013.
 Banana Zoro na kundi zima la B Band lilitoa burudani.
 Kazi ni kwako
 Mambo ya burudani yalikuwa si mchezo, Uncle Lundenga na my wife wake wakisakata rhumba toka B Band.
 Wadau wa Miss Tanzania walikuwepo kuunga mkono uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Excutive Solutions, Aggrey Maliale akibadilishana mawazo na Meneja Masoko wa TBL, Mamungai.
 Mdau na Mwandaaji wa Miss Musoma, Godson Mukama (kulia) akiteta jambo na Fimbo Butala wa TBL.
 Warembo hii ilikuwa shughuli yao.
 Kamati ya Miss Tanzania ikiwa katika picha ya pamoja.
 Warembo ndani ya uzinduzi huo wa Miss Tanzania 2013.
Wadau mbalimbali wa sanaa ya urembo wakiwa ndani ya Serena Hoteli kushuhudia Uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.