Habari za Punde

*WAKATOLIKI WAPATA PAPA MPYA FRANCIS WA KWANZA

 Papa Francis wa kwanza.

Moshi mweupe.
Baada ya kusubiriwa kwa hamu kubwa kupatikana kwa Papa mpya wa kuliongoza kanisa la Katoliki, hatimaye Jopo la Makardinali 115 wa Kanisa hilo, wamemchagua Kardinali wa Buenos Aires kutoka Latin Amerika, Jorge Mario Bergoglio (76) kuwa kiongozi mpya atakaye chukuwa nafasi ya  Papa Benedict aliyejiuzulu siku za hivi karibuni.

Jorge Mario Bergoglio, ambaye ni Muagrgentina tayari amechagua jina atakalotumia katika kipindi chake cha Uongozi kuwa anapendelea kuitwa Papa Francis.

Jopo hilo limemteua Cardinal Jorge Mario Bergoglio, kushika wadhifa huo mpya wa  Papa katika uchaguzi uliofanyika kwa mara ya tano kwa kura zilizopigwa na Makadinali 115 waliokuwa wakikutana katika kanisa la Sistine Chapel huko Vatican , Roma.

Maelfu ya watu walikuwa wamefurika katika eneo la la St. Peters huko Vatican huku mamilioni wengine wakishuhudia Papa huyo mpya akitangzawa mbele yao.


Papa Francis ni Papa wa Kwanza kuchaguliwa kutoka Latin America tangu kuanzishwa kwa Kanisa Katoliki Duniani.

Aliwahi pia kutajwa kumrithi Papa John Paul II wakati wa kumtafuta Papa na akashinda Papa Benedict ambaye amejiuzulu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.