Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam anayechukua masomo ya sayansi, Halima Ahmad akichangia hotuba ya mwisho wa mwezi aliyoitoa Rais Kikwete kuhusu amani na utulivu nchini , amesema wanavyuo wasikubali kutumiwa katika kuleta migogoro isiyokuwa na manuafaa kwa taifa letu, bali waendelee kutafuta elimu kwa faida yao pamoja na maendeleo nchini.
Mwinjilisti wa kanisa la Divin Wisdom la Jijini Dar es Salaam Hance Buntuntu (pichani) akitoa maoni yake kwa waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu hotuba ya mwisho wa mwezi alioitoa Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni akizungumzia uhusiano wa Wakristu na Waislamu, ambapo Mwinjilisti huyo amesema anasikitishwa kuona hali imebadilika ya maisha ya upendo kati ya dini hizi na amewashauri wananchi waendelee kuishi kwa amani kwani sote ni Watanzania.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Taifa na Mwenyekiti wa tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM )Seki Kasuga pichani akitoa maoni yake kuhusu hotuba ya mwisho wa mwezi aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni, Seki amewashauri wanavyuo nchini kutobaguana, kushikamana ili kuendelea vizuri kwenye masomo yao pamoja na kujiepusha vitendo vitakavyoleta migogoro.
Muhibiri wa Dini ya Kiislamu Said Mwaipopo (pichani) akichangia kutoa maoni yake kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam(hawapo pichani) na kukemea baadhi ya watu wanaovuruga amani kwa vitendo visivyofaa vya kuleta udini, nchi yetu ni huru tuendelee kuishi kwa amani.Pia ameunga mkono hotuba ya Mh. Rais Jakaya Kikwete. Picha zote na Mwanakombo Jumaa- (MAELEZO).
No comments:
Post a Comment