Habari za Punde

*EXTRA BONGO YAZIDI KUPASUA ANGA, KUTAMBULISHA WAWILI WAPYA APRIL 15

Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choki (kushoto) akimsikiliza mpiga solo wake, Ephraem Joshua, wakati akilikung'uta solo hilo kwenye Onyesho la bendi hiyo linalofanyika kila siku ya Jumapili katika viwanja vya Garden Breeze Magomeni. Bendi hiyo inatarajia kuendelea kujiimarisha kwa kuongeza wanamuziki wapya, ambapo inatarajia kutambulisha wanamuziki wawili watakaojiunga na bendi hiyo wakitokea katika moja ya bendi kubwa nchini ambayo Mkurugenzi huyo hakupenda kuiweka wazi jina la bendi hiyo watakapotoka wanamuzikihao. Utambulisho wa wanamuziki hao unatarajia kufanyika katika onyesho maalum la bendi hiyo litakalofanyika April 15.
 Muimbanji wa Bendi ya Extra Bongo, Banza Stone akicheza pamoja na wanenguaji wa kike wa bendi hiyo, wakati wa onyesho la Bendi hiyo katika Viwanja vya Garden Breeze Magomeni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, iliyopita.

 Rapa wa Extra Bongo,Frank Kabatano(kushoto) akiimba sambamba na mpiga Bass, Hoseah Mgoachi wakati wa onyesho la Bendi hiyo katika Viwanja vya Garden Breeze Magomeni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wanenguaji  wa Extra Bongo,wakishambulia jukwaa.
Rapa wa Extra Bongo,Frank Kabatano akicheza zambamba na mcheza wakati wa onyesho la Bendi hiyo katika Viwanja vya Garden Breeze Magomeni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.