Habari za Punde

*KAMUHANDA -ELIMU YA UZALENDO IMECHANGIA NCHI KUWA NA MANI NA UTULIVU

NA MAGRETH    KINABO
ELIMU ya uzalendo imesaidia  kuwafanya  vijana  wa Kitanzania kuipenda nchi yao , hali iliyochangia nchi yetu kuwa na amani na utulivu.
Kauli hiyo ilitolewa leo na  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na  Michezo,Seth Kamuhanda wakati akizungumza na ujumbe wa  watu 22,baadhi yao ni viongozi wa utawala na 13 ni wanafunzi wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu wa mafunzo ya   kijeshi  kutoka  Nigeria.
Ujumbe huo umetembelea wizara hiyo kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali ya  Utamaduni wa Kitanzania, umeongozwa na kiongozi wa msafara, Meja  Generali, Ati  John,ambaye ni Mkurugenzi wa Jeshi la Wanamaji.
“Mojawapo ya program tunazowafundisha  vijana ili kuondoa  migogoro  katika nchi  yetu ni elimu ya uzalendo ,yaani tunawafundisha jinsi ya kuipenda nchi yao. Elimu hii imesaidia  kupunguza migogoro,alisema.” Katibu Mkuu huyo alipokuwa akijibu swali la mmoja ya wanafunzi  hao   lililouliza kuwa  kuna program  zipi zinazochangia kupunguza migogoro  hususan kwa vijana.
Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa kuna mkakati wa kuwawezesha vijana kiuchumi ili waweze kubuni miradi mbalimbali kwa kuwa na mfuko wa vijana.
Alisema katika mpango huo vijana wanakuwa katika vikundi na kufanya shughuli  mbalimbali  kuwawezesha kiuchumi.
Aidha Katibu Mkuu huyo akizungumza kuhusu masuala ya kiutamaduni ,alisema wizara  yake ndi yenye jukumu lakuendeleza Utamaduni wa Mtanzania, hivyo katikawizara hiyo yenye sekta nne, ambazo ni Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
 Kamuhanda  alisema sektaya utamuduni ndio inayofanyakazi ya kudumisha Utamaduni huo.
 Aliongeza kuwa lugha ya Kiswahili ndio imekuwa lugha kuu ya mawasiliano nchini  na ndiyo iliyoleta umoja ,amani na mshikamano.
 Wakizungumzia kuhusu ziara hiyo kiongozi huyo na mmoja wa wanafunzi,  Ikema Francis walisema wameshukuru kwa taarifa walizopata kuhusu wa masuala hayo ya kiutamaduni na kuhafamu kuwa lugha ya Kiswahili ndiyo imeleta umoja.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.