Habari za Punde

*KANISA LA WESTMINISTER ABBEY LA LONDON LAONGOZA MISA MAALUM YA KULIOMBEA TAIFA LA TANZANIA

 Mh Balozi Kallaghe (kulia) akisalimiana Kiongozi wa Kanisa baada ya ibada maalum ya kuliombea Taifa la Tanzania siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa kutimiza miaka 49, iliyoadhimishwa hivi karibuni, huku ibada hiyo ikiwajumuisha na watu wengine wa Mataifa mengine waishio nchini humo.
  Balozi wetu Mh Peter Kallaghe, maofisa kutoka ubalozini wa Tanzania nchini Uingereza na baadhi ya watanzania waishio nchini Uingereza walijumuika kwa pamoja kuhudhuria ibada maalum na raia wengine kutoka nchi mbalimbali.  Ibada ilianza kwa jumuiya ya Abbey kuwaombea  watanzania wote, viongozi pamoja na wanadiplomasia wote waliopo duniani na kwa ajili ya kazi maalum ya Ubalozi wetu nchini Uingereza.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA

 Mh Peter Kallaghe na Frank Eyembe.

 Picha ya pamoja baada ya Ibada hiyo maalum, iliyofanyika katika Kanisa la Westminister Abbey, London.
 Kanisa hilo la Westminister Abbey, lililofanyikia ibada hiyo.
 Kutoka kushoto Abu Faraji, Caroline Chipeta, Mirium Mungula na mdau baada ya ibada.
Wazee wa Kazi wakipozi kwa picha.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.