Habari za Punde

*KINANA, NAPE WAFUNIKA ZIARA YAO YA KILOMBERO

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akivishwa skafu na chipukizi alipowasili  eneo la kivuko cha Kilombero tayari kuanza ziara ya kikazi ya kuimarisha uhai wa chama hicho katika Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro,Kinana alikuwa akitokea wilayani Ulanga.PICHA NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA
 Wanachama wa CCM wakiimba wimbo wa kumkaribisha wilaya ya Kilombero Katibu Mkuu wa CCM Andulrahman Kinana, akitokea wilaya ya Ulanga pamoja na vingozi wengine wa chama hicho.
Katibu Mkuu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akipandisha bendera kuzindua rasmi Tawi la CCM la Manjecha  eneo la Mahutanga, wilayani Kilombero.
 Katibu Mkuu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa na watoto waliokuwa sehemu ya watu walioshuhudia  uzinduzi wa Tawi la CCM la Manjecha  eneo la Mahutanga, wilayani Kilombero.

 Katibu Mkuu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akipandisha bendera kuzindua rasmi Tawi la CCM la Manjecha  eneo la Mahutanga, wilayani Kilombero
Ranfred Majiji ambaye alikuwa mfuasi wa Chadema akikabidhiwa kadi ya CCM na Kinana.
 Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Ifarakara Mjini
Sehemu ya umati wa wananchi uliofika kwenye mkutano huo
 Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Elias Masala (kulia), akijibu maswali mbele ya Kinana jinsi alivyopanga mikakati ya kuwaletea mandeleo wananchi wa wilaya hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), akimkabidhi ubani mtoto wa aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilombero, marehemu Oswald Mkokochela, Edward wakati uongozi wa chama hicho ulipokwenda jana  kuifariji familia kwa msiba wa uliotokea juzi. Ifakara Mjini.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.