Habari za Punde

*KUMBUKUMBU NA KISOMO CHA YA HITIMA YA MZEE KARUME LEO MJINI ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,akisalimiana na wakuu wa Vikosi vya ulinzi alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisdiwandui Mjini Unguja kuhudhuria katika Hitma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.

Askari wakijipanga kupoea viongozi waliokuwa wakiwasili mahala hapo.
Rais Jakaya Kikwete, akiweka Shada la Maua katika kaburi, wakati wa shughuli hiyo.
Mjukuu akiweka Shada la maua katika kaburi.
Rais Jakaya Kikwete, akiwaongoza makamu wake na Rais wa Zanzibar, na viongozi wengine kuomba dua wakati wa shughuli hiyo.
Sehemu ya Wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislamu waliohudhuria kisomo cha Hitima Kumuombea Dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya CCm Kisiwandui Mjini Zanzibar,ambapo kila ikifika siku kama hii wananchi kwa ujumla wao hukusanyika kuomba dua kama hii.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wakuu wa Vikosi vya ulinzi alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisdiwandui Mjini Unguja kuhudhuria katika Hitma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.Zaidi Bofya HAPA chini
Wake wa Viongozi Wakuu wakiwemo na viongozi wa taasisi za Kinamama wakinyanyua mikono juu kumuombea dua  Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.katika kaburi lake huko CCM Kisiwandui mjini Zanzibar,baada ya kisomo cha Hitma leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na wakuu wa Vikosi vya ulinzi alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisdiwandui Mjini Unguja kuhudhuria katika Hitma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume
Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume,(kulia) akiwa na Wake wa Viongozi mbali mbali katika Hitma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,huko Ukumbi wa CCK Kisiwandui Mjini Zanzibar Leo.
Akina mama wa Kiislamu wa Mjini Magharibi Unguja wakijumuika na Viongozi wengine katika kisomo cha HItmaya Kumuombea Dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.