NDUGU, Jamaa na marafiki wa aliyekuwa Nguli wa Filamu nchini,
Stive Kanumba, leo wamejumuika kwa pamoja katika kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu staa huyo wa filamu alipofariki
dunia.
Ikiwa ni mwaka mmoja tangu kutokea kwa msiba huo, leo pia
mashabiki wa filamu za kibongo waliohudhuria hafla ya
kumbukumbu hiyo kwa pamoja kuweka mashada ya maua katika
kaburi la Kanumba, wamewashuhudia Mama Kanumba na
Msanii Elizabeth Michael 'Lulu' wakiungana na kuwa kitu kimoja
na kuondoa tofauti zao na kuadhimisha kumbukumbu hiyo kwa
kuwaongoza watu waliohudhuria.
Katika Hafla hiyo walihudhuria pia wasanii kibao wa Filam, ambao
pia walipata fulsa ya kuweka mashada ya maua.
|
No comments:
Post a Comment