Habari za Punde

*MKUU WA MKOA WA PWANI MHE. MWANTUMU MAHIZA ATEULIWA KUWA SKAUTI MKUU TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza kuwa Skauti Mkuu nchini.
Kwa mujibu wa barua ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue  amesema uteuzi wa Mheshimiwa Mahiza umeanza tangu tarehe 19 Aprili, 2013.
Mheshimiwa Mahiza anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kanali Mstaafu Iddi Kipingu ambaye amemaliza muda wake.

Imetolewa na:
KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.