Pamoja na ushindi huo wa Madrid ya Hispania kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, lakini bado timu hiyo ime imeondoshwa kwenye mashindano hayo ya UEFA kwa jumla ya mabao 4-3, kutokana na mchezo wa kwanza uliochezwa wiki iliyopitwa ambapo Borussia Dortmund, waliichapa Madrid mabao 4-1.
Mabao ya Madrid yalifungwa na Benzema katika dakika ya 82 na Ramos katika dakika ya 88.
Kwa matokeo hayo sasa Borussian Dortmund wamefuzu kutinga fainali ya michuano hiyo jumla ya mabao 4-3, ambapo sasa wanasubiri matokeo ya mchezo wa leo kati ya Barcelona na Bayern Munich, ambao nao katika mchezo wa kwanza, Barca walilala kwa mabao 4-0.
Mtanange ukiendelea......
Ronaldo (kulia) akijaribu kumtoka Braszczykowsk, wakati wa mchezo huo.
Nahodha wa Timu ya Madrid, Sergio Ramos (kushoto) akishangilia na Karim Benzema, baada ya kuifungia timu yake bao wakati wa mchezo wa Nusu fainali wa Ligi ya Mabingwa uliochewza jana usiku kati yao na Borussia Dortmund. Katika mchezo huo Madris iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

No comments:
Post a Comment