Habari za Punde

*SPIKA WA BUNGE ANNE MAKINDA AWAASA WABUNGE KUTUMIA LUGHA YA STAHA MJENGONI

 Spika wa Bunge Anne Makinda awaasa Wabunge kutumia Lugha ya Staha ambayo ni ya Kibunge wakati wa kuchangia mijadala Bungeni. Mhe. Makinda amesema, kuendelea kutumia lugha ya matusi, kejeli na maudhi kwa baadhi ya Waheshimiwa Wabunge ni kuendelea kuliondolea hadhi Bunge. 

Pamoja na hilo, wabunge wanatakiwa kujikita katika kuchangia hoja zenye kutataua matatizo ya wananchi ili kutimiza wajibu wa kila mbunge wa kuwa wakilisha wananchi. 

Mhe. Makinda , amesema, fursa ya kila Mbunge kuchangia lazima ilenge kutatua matatizo ya wananchi na sio kutukanana na kusahahu jukumu lilomblele ya kila Mbunge. 

Katika Picha ni baadhi ya waheshimiwa Wabunge waliochangia mjadala wa kupitisha Makadirio na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2013/14 Mjini Dodoma.
 Mbunge wa Mwibara Mhe. Kangi Lugola, akiomba Mwongozo kwa Spika Bungeni.
 Mbunge wa Ukerewe Mhe. Salvatory Machemli akichangia Mjadala Bungeni leo.
 Mbunge wa Viti Maalum (CUF) Mhe. Kuruthum Mchuchuli akichangia  kwa hisia mjadala leo Bungeni.
 Mbunge wa Temeke Mhe. Abbas Mtembu akichangia Mjadala.
 Waziri Mkuu Msaafu Mhe. Edward Lowasa akifuatilia kwa makini Mijadala Bungeni leo.
 Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na teknolojia Mhe. January Makamba akijibu baadhi ya hoja zilizochangiwa Bungeni leo.
 Mhe. Catherine Magige, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) akichangia Mjadala leo. Picha Zote na Picha na Ofisi ya Bunge

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.