Habari za Punde

*WAZIRI DKT. MUKANGARA AKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akibadilishana kadi ya mawasiliano (Business Card) na Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose alipomtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam. Ubalozi wa Uingereza umeahidi  kushirikiana na wizara hiyo katika sekta ya Vijana, Utamaduni, Michezo na  kuendelea kutoa mafunzo kwa maafisa habari wa Serikali na Taasisi zake.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akimshukuru  Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose kutokana na ubalozi huo kutoa mafunzo ya mitandao ya kijamii (Social Media)  kwa maafisa Habari wa Serikali na Taasisi zake yaliyofanyika mwezi wa tatu mwaka huu. Balozi huyo alimtembelea waziri Dk. Mukangara ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumsalimia na kuimarisha mahusiano baina ya  Wizara hiyo na Uingereza.  

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akisalimiana  na Joseph Paync  ambaye ni afisa miradi kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini  alipomtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Uingereza nchini Dianna Melrose.  Picha na Anna Nkinda - Maelezo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.