Habari za Punde

*YANGA INAONGOZA MABAO 3-0 DHIDI YA JKT OLJORO

 Kipa wa JKT Oljoro, Lucheke Mussa, akipangua mpira wa kona uliopigwa na Haruna Niyonzima, ambao ulirudishwa na kimakosa na beki wake na kutupiwa nyavuni na Nadir Haroub 'Canavaro' katika dakika ya 4 ya mchezo na kuandika bao la kwanza. Bao la pili lilifungwa na Simo Msuva baada ya kuwachambua mabeki wa Oljoro na kuachia shuti la mbali kama mita 19, katika dakika ya 16, huku bao la tatu likitupiwa nyavuni na Hamis Kiiza katika dakika ya 43 kufuatia pasi nzuri ya Haruna Niyonzima.
Nadir Haroub 'Canavaro' akitupia bao lake la kwanza la kuongoza wakati wa mchezo huo kipindi cha kwanza. Hivi sasa mpira ni kipindi cha pili.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.