Habari za Punde

*YANGA YASUBIRI POINTI 1 TU KUTANGAZA UBINGWA, JE KUTANGAZIA KWA COASTAL UNION? YAICHAPA JKT RUVU 3-0

Wachezaji wa Yanga, wakimpongeza mwenzao, Simon Msuva baada ya kuifungia  timu yake bao la kwanza dhidi ya JKT Ruvu, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.
 Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 3-0, huku bao la kwanza likifungwa na Simon Msuva, la pili Hamis Kiiza na la tatu likitupiwa na Nizar Khalfan. 
Kwa matokeo hayo sasa Yanga imebakiza pointi moja tu ili kutangaza ubingwa rasmi, kutegemea na mchezo wa Jumatano kati ya Azam Fc na Coastal Union, huku ikiwa iebakiza michezo miwili unaofuata ukiwa ni kati yao na Coastal Union kutoka Tanga na mchezo wa mwisho ukiwa ni ule unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchi kati yao na Watani wao wa Jadi Simba, unaotarajia kpigwa mwezi ujao.
Mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva (kulia) akimtoka beki wa JKT Ruvu,  Damas Makwaya, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa ,Dar es Salaam leo jioni. Yanga imeshinda mabao 3-0.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.