Habari za Punde

*MASHALI 'CHALI' AKUBALI YAISHE ACHAPWA RAUNDI YA 10, AKUBALI CHEKA KUONDOKA NA NOAH

 Mwamuzi wa pambano la masumbwi kati ya Francis Cheka (aliyesimama) na Thomas Mashali, akimwesabia Mashali baadda ya kuchapwa konde takatifu na mpinzani wake, lililompeleka chini katika raundi ya 10 na kushindwa kuinuka na kuendelea na pambano, wakati wa pambano lao lililomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba. Pambano lilikuwa ni la kukata na shoka kwa pande zote mbili zikishambuliana kwa zamu na makonde mazito yaliyosisimua.
 Thomas Mashali (kulia) akirushiana makonde na mpinzani wake Francis Cheka, wakati wa pambano hilo.
Mwamuzi akimzuia Mashali kuinuka baada ya kuona kuwa alikuwa amezidiwa huku akipepesuka kila alipojaribu kuinuka.
*****************************
Na Ripota wa Sufianimafoto
BONDIA Machachari, Francis Cheka 'Mbishi', leo tena ameendeleza ubabe wake kwa kuendelea kuwachapa mabondia wa nyumbani kwa K/O.

Katika Pambano lake na mpinzani wake Thomas  Mashali, lililokuwa na upinzani mkubwa huku kila bondia akishambulia kwa kupokezana, Cheka aliweza 'kumkalisha' Mashali katika raundi ya 10 katika pambano lao la raundi 12 la Ubingwa wa IBF.

Pambano hilo lililomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba, limehudhuriwa na mashabiki lukuki waliovunja rekodi ya kujaa katika ukumbi huo, jambo lililowafanya waandaaji kufungua Geti kubwa na kuacha wazi huku mashabiki walioshindwa kuingia ndani wakiendelea kupata burudani hiyo wakiwa wamesimama kwa nje ya ukumbi huo.

Cheka alifanikiwa kumpeleka chini mpinzania wake mara mbili katika raundi ya kwanza na ya nne kabla ya kumaliza pambano hilo katika raundi ya 10.

Mara baada ya kuangushwa Mashali, alionekana kukata tamaa huku akiwa kama amepoteza fahamu, jambo lililomfanya mwamuzi wa pambano hilo kuamua kumaliza.

Kwa ushindi huo sasa, Cheka anatarajia kuakabidhiwa gari lake aina ya Noah kesho majira ya saa nne asubuhi pamoja na mkanda wa IBF, huku akiandaliwa pambano moja la kutetea ubingwa huo na bondia kutoka nje ya nchi.

KWA PICHA ZA MATUKIO KIBAO YA PAMBANO HILI LILILOKUWA NA KILA AINA YA VITUKO NA UPINZANI MKUBWA, USIKOSE KUTEMBELEA UKURASA HUU HAPO BAADAYE.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.