Kipa wa Coastal Union, Shaban Kado (kushoto) akilala kuokoa mpira mbele ya mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jioni ya leo. Katikati ni beki wa Coastal, Yusuph Chuma, akijiandaa kutoa msaada. Katioka mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya 1-1, huku mabao yote yakifungwa katika kipindi cha kwanza. Bao la Yanga limefungwa na Jerry Tegete katika dakika ya 4, baada ya kuwaramba chenga mabeki na kipa wa Coastal, na la Coastal, likifungwa na Abdi Banda, kwa mpira wa faulo.
Mtanange ukiendelea, ni Kijana mdogo wa Timu B ya Yanga, Abdallah Mguli, akimkalisha beki wa Coastal, Yusuoh Chuma, wakati wa mtanange huo.
Huku nje nako askari walikuwa imara kuimarisha ulinzi, hapa wakimdhibiti mmoja wa vijana waliyemkamata akiuza tiketi feki nje ya uwanja.
Mashabiki wa Yanga, wakiingia na Kombe lao la mfano uwanjani.
Askari wakiwadhibiti na kuwaweka chini ya ulinzi vijana waliowakamata wakiuza tiketi feki.
Mashabiki wa Yanga, wakiingia na Kombe lao la mfano uwanjani.






No comments:
Post a Comment