Habari za Punde

*BALOZI IDDI ATEMBELEA HOTELI YA SUN SET BUNGALOWS ILIYOUNGUA MOTO MJINI ZANZIBAR

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na Mmiliki wa Hoteli ya Sun Set Bungalows iliyoko katika Kijiji cha Kendwa Nungwi Abdullsamab Ahed Said akikagua athari iliyosababishwa na moto mkubwa uliyoyakumba baadhi ya majengo ya Hoteli hiyo juzi jioni. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “A” Machano Fadhil Machano (Babla)  na Nyuma yao aliyevaa suti za Bahari ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk.
 Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja  Pembe Juma Khamis akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  hali halisi ya moto ulivyoikumba  Hoteli ya White Sand iliyoko Kendwa Nungwi Mkoani humo juzi jioni.
Baadhi ya Majengo ya Hoteli ya White Sand iliyopo pembezoni mwa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Kendwa Nungwi ikiwa ni miongoni mwa majengo 10 ya hoteli hiyo yaliyoteketea kwa moto mapaa yake juzi jioni. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.