Afisa Afya wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mohamed Kiula, akieleza hali ya utekelezaji wa Kampeni ya Afya na usafi wa mazingira katika wilaya ya Kishapu kwa wananchi na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N.Rufunga mapema wiki hii alipofanya ziara wilayani hapo katika kijiji cha Bupigi kata ya Uchunga, kukagua utekelezaji wa kampeni hiyo ikiwa ni maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete kuhamasisha jamii kubadili tabia na mtazamo wa jamii katika kutathmini suala la usafi wa mazingira.
Na Magdalena Nkulu
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga aliyofanya kwenye Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Halmashauri ya Mji Kahama pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Ushetu ametoa rai kwa wananchi kutizama upya suala la mila na desturi kwa baadhi ya makabila kutotumia choo kimoja na wakwe linasababisha uchafuzi wa mazingira kwani inabidi wakati fulani wakwe kujisaidia vichakani pale wanapotembelewa na wakwe zao.
Hivyo amewataka wananchi kuacha mila hizo kwani hakuna madhara yoyote,vinginevyo kaya hizo ziwe na vyoo viwili.
Amewataka pia viongozi hasa Wakuu wa wilaya kusimamia sheria ya uchafu wa mazingira inayomfunga mtu yeyote mwenye kosa hilo kwa mwaka mmoja au faini ya Tsh.Milioni moja.
Mkuu wa Mkoa ametembelea vijiji vya Bupigi wilaya ya Kishapu, Mpunze Halmashauri ya wilaya ya Ushetu na Nyamilangano katika Halmashauri ya Mji Kahama ili kuona hali ya utekelezaji wa kampeni hiyo.
No comments:
Post a Comment