Habari za Punde

*RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AMUAPISHA MSHAM ABDULLA KHAMIS KUWA NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA UWEZESHAJI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Msham Abdula Khamis kuwa Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Unguja leo asubuhi.
 Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana na Viongozi wakati alipohudhuria katika ukumbi wa Ikulu  Mjini Unguja, wakati wa  hafla ya kuapishwa  Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto,Msham Abdula Khamis, leo asubuhi.
 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora, Dk.Mwinyihaji Makame,Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar
Kabi na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji,wakiwa ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa  Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto, Msham Abdula Khamis.
 Mawaziri wa Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu  Mjini
Unguja, wakati wa  hafla ya kuapishwa  Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Vijana,Wanawake na Watoto,Msham Abdula Khamis,leo asubuhi.

 Makamo wa kwanza wa Rais Maalim  Seif Sharif Hamad,akisalimiana na Viongozi wakati alipohudhuria katika ukumbi wa Ikulu  Mjini Unguja, wakati wa  hafla ya kuapishwa  Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii, Vijana,Wanawake na Watoto,Msham Abdula Khamis,leo asubuhi. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.