Habari za Punde

*UFUNGUZI WA WARSHA YA UANDAAJI MKAKATI WA NISHATI TUNGAMOTO (BIOMASS)

 Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava (kushito) akisalimiana na Mike Bess ambaye ni mshauri na mmoja wa waanzilishi wa Shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia mazingira na nishati jadilifu (CAMCO) wakati wa warsha ya siku moja ya kujadili uandaaji mkakati wa nishati – tungamotaka (Biomass) nchini inayofanyika leo katika Hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava akiongea na washiriki wa  warsha ya kujadili uandaaji mkakati wa nishati – tungamotaka (Biomass) nchini inayofanyika leo katika Hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo ya siku moja imeandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia mazingira na nishati jadilifu nchini (CAMCO).
Baadhi ya washiriki wa warsha ya siku moja ya kujadili uandaaji mkakati wa nishati – tungamotaka (Biomass) nchini wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava (hayupo pichani) wakati akifungua warsha ya siku moja ya kujadili uandaaji mkakati wa nishati – tungamotaka (Biomass) nchini leo katika Hoteli  ya Colosseum jijini Dar es Salaam. Hivi sasa Serikali iko katika mchakato wa kubadilisha sera ya nishati ili iweze kutekeleza mkakati wa tungamotaka.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.