Waziri wa Manedeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia
Simba akitoa maelezo juu ya kauli zenye kuashiria uvunjifu wa sheria na tabia
za vurugu katika jamii ambazo zilitolewa na baadhi ya wanasiasa hivi karibuni
katika vyombo vya habari hapa nchini.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa
Manedeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba wakati akitoa maelezo
juu ya kauli zenye kuashiria uvunjifu wa sheria na tabia za vurugu katika jamii
ambazo zilitolewa na baadhi ya wanasiasa hivi karibuni katika vyombo vya habari
hapa nchini. PICHA NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO
****************************
Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO-Dar es Salaam.
SERIKALI
imeshtushwa na baadhi ya ujumbe wa maneno uliopelekwa kwa wananchi na baadhi ya
vyama vya siasa hapa nchini ambao unaweza kuleta kuhatarisha amani na usalama
wa Tanzania.
Kauli hiyo imetolewa na
Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Sophia Simba leo jijini
Dar es salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake.
Waziri Simba amesema
kuwa kauli zilizotolewa hivi karibuni na baadhi ya vyama vya siasa vilivyofanya
mkutano wa hadhara katika viwanja vya Jangwani zimeishtua Serikali na zinaweza
kuleta madhara makubwa kwa jamii hususani wanawake, wazee, walemavu na watoto.
Waziri Simba amesema kauli
zilizotolewa na viongozi hao ni pamoja na “Vijana msikubali wakati wa kufanya
mazoezi umefika” kauli hii inahitaji tafakari na kuhoji kwa makini
inawahamasisha vijana kutii, jambo ambalo linaweza kuwafanya walete vurugu.
Amesema kuwa kauli hiyo
na nyingine zilizotolewa na viongozi hao wa juu wa vyama hivyo zinazowachochea
wananchi kutotii na ni ishara ya uwepo
wa njama mbaya za kuwashawishi wananchi ili siku hiyo wajichukulie sheria
mikononi, kinyume cha katiba, sheria na haki za binadamu.
Aidha, Waziri Simba alisema
jamii inahitaji kutafakari juu ya kauli hizo na mustakabali wa Tanzania.
Amesema kuwa jamii ya
Watanzania inatakiwa kutambua kuwa amani na usalama ndio mtaji namba moja wa
maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kidemokrasia. Ustawi wa jamii ya Watanzania
unahitaji amani, utulivu na usalama.
No comments:
Post a Comment