
Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO Getrude Sima (kushoto) akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba (kulia) kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya siku sita kuhusu maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake wasiokuwa kwenye ajira rasmi na wanaoishi pembezoni katika juhudi za kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.
Zaidi ya wanawake 220 wafikiwa na mradi huo wa Shirika la Kazi Duniani

Mshauri wa Biashara wa shirika lisilokuwa la Kiserikali (NGO) TAPBDS Bi. Theresia Kato akifundisha wakinamama wa Chalinze (hawapo pichani) jinsi ya kuandika na kuandaa mchanganuo wa biashara katika mafunzo hayo ya siku sita yaliyoandaliwa na Shirika la kazi Duniani (ILO).


Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO Bi. Getrude Sima akisisitiza jambo kwa washiriki kuhusiana na mafunzo waliyoyapata yakawe chachu ya kuleta maendeleo.

![]() |
Picha juu na chini ni baadhi ya wakinamama wa Chalinze wakifuatilia mafunzo hayo yaliyomalizika mwishoni mwa wiki. |

Mgeni rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba akikabidhi vyeti kwa mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo.

Mwanamke wa Kimasai Paspen Kisota akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo hayo.

![]() |
Picha juu na chini mgeni rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba na Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO Getrude Sima wakiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu. |

Fundi Sanifu wa Maabara ya Afya Bw. Rwezahura Merehiory akichukua damu kwa ajili ya vipimo vya VVU kwa mmoja wa washiriki wa semina ya mafunzo ya Ujasiriamali na Kupambana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi iliyoratibiwa na shirika la Kazi duniani (ILO) wilaya ya Chalinze mwishoni mwa wiki.
**********************************************************************
Na Damas Makangale, Chalinze
SHIRIKA
LA KAZI DUNIANI (ILO) limeendesha mafunzo ya siku sita kuhusu
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake wasiokuwa kwenye ajira
rasmi na wanaoishi pembezoni katika juhudi za kudhibiti maambukizi mapya
ya Virusi vya Ukimwi.
Mradi
huo wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) unalenga wanawake wote ambao wapo
pembezoni wa barabara na mipakani kwa sababu wapo katika hali ya
hatarishi.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Mkoa Pwani Wilayani Chalinze, Mratibu Msaidizi
wa Mradi wa Ukimwi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Getrude Sima
amesema ndani ya siku sita mradi wa mapambano ya Ukimwi chini ya ILO
umewafikia wanawake 120 katika kata za Pera, Chamakweza, Mpingo,
Bwilingu, Msolwa na Mdaula.
Alisema
tangu mradi uanze kutekelezwa hapa nchini wakutoa mafunzo ya
ujasiriamali na kujikinga na Virusi vya Ukimwi wameweza kuwafikia
wanawake 220 nchi nzima katika maeneo ya pembezoni na mpakani kama vile
Tunduma, Kyela na Namanga.
“Unajua
wanawake wengi wanakuwa katika kundi hatarishi pale wanapokuwa katika
maeneo ya mpakani na pembezoni mwa barabara kwa mfano Chalinze kwa
sababu ya muingiliano wa watu hasa Madereva na Wafanyabiashara,” alisema
Sima.
Sima
aliongeza kuwa katika mradi huu wa mapambano ya Ukimwi malengo ni
kumuelimisha Mwanamke ili ajitambue na aweze kujikinga na maambukizi ya
Virusi vya Ukimwi kwa kumfundisha stadi za maisha pamoja na
ujasiriamali.
Alisema
mradi unalenga wanawake wasiokuwa katik ajira rasmi ili kuongeza
muamuko miongoni mwa wakinamama mitaani na vijijini ili waweze
kukabiliana na vishawishi katika sehemu zao wanazoishi.
Kwa
upande Mshauri wa Biashara toka shirika lisilo kuwa la Kiserikali
TAPBDS, Theresia Kato alisema kuwa biashara ndogo ndogo ni muhimu katika
kumjengea mwanamke uwezo wa kujiamini na kujitegemea.
“lazima
wanawake waamuke ili waweze kuanzisha biashara zao na kuandika
mchanganuo wa biashara na kutafuta mitaji kupitia taasisi mbalimbali za
fedha hapa nchini,” alisema.
No comments:
Post a Comment