Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika wakati alipohudhuria katika Mkutano wa mkuu wa tatu wa nchi za Kiarabu, 'Afro Arab' uliofanyika leo, nchini KUwait.
Makamu
wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozana na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika, wakati wakiwasili
kwenye ukumbi wa Mkutano wa Tatu wa nchi za Kiarabu 'Afro Arab',
uliofanyika nchini Kuwait, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa sita kutoka kushoto, mstari wa tatu nyuma) akihudhuria mkutano mkuu wa tatu wa nchi za Kiarabu, 'Afro Arab' uliofanyika leo Nov 19, 2013, nchini Kuwait.
Hadha waliyopata wapiga picha wakati wa kuingia ukumbi humo kwa ajili ya kupata matukio ya mkutano huo ikiwa ni pamoja na kupata picha za viongozi wa nchi, zao, ambapo wapiga picha hao walilazimika kutumia nguvu kwa kuwasukuma askari na kuazidi nguvu na kisha kuingia ndani baada ya askari hao kutokua na utaratibu mzuri wa kuwaongoza wapigapicha. Askari hao walikuwa wakiwafukuza wapiga picha huku wakiwataka kupanga foleni, na wanapofanya hivyo hughairi na kuwataka warejee katika chumba cha wanahabari ili waanze kuita mmoja baada ya mwingine, jambo ambalo lilionekana kuwa usumbufu. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Wapiga picha wakiwa tayari wamevamia mlango mkuu wa kuingilia ukumbini humo huku wakisukumana na kuwazidi nguvu askari na kufanikiwa kuingia ndani.
Hapa wakiwa katika mlango wa tatu wa kuingia ndani ya ukumbi huo, baada ya kuwazidi nguvu askari wa mlango wa kwanza na wa pili.
********************************
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL, AIWAKILISHA
TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA AFRO – ARAB NCHINI KUWAIT
Kuwait City, Novemba 19, 2013
Makamu wa Rais wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt
Mohammed Gharib Bilal ameiwakilisha Tanzania katika mkutano wa mashirikiano
baina ya nchi za Afrika na zile za Kiarabu, mkutano wa siku mbili unaofanyika
katika nchini Kuwait. Mkutano huo unaohudhuriwa na viongozi wa nchi zaidi ya 70
unalenga kuimarisha ushirikiano wa Afrika na nchi za Kiarabu na unapitia
makubaliano ya mkutano wa Sirte, Libya uliofanyika mwaka 2011.
Mkutano huu unafanyika kukiwa na mabadiliko kadhaa ya
kiasiasa, kiuchumi na kimkakati baina ya nchi za kanda hizi mbili huku taswira
ya kukua kwa ushikiano huu zikionekana bayana kuwa muhimu zaidi sasa kuliko
ilivyokuwa huko nyuma. Hii inatokana na nchi za kanda hizi mbili, kukabiliwa na
changamoto nyingi zinazofanana na zinazohitaji majibu ya pamoja baina ya nchi
za kanda hizi mbili. Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na; mtikisiko wa
uchumi, hali ya ulinzi na usalama, majanga yanayoikabili dunia, usalama wa
chakula na ugaidi.
“Changamoto hizi hatuwezi kuzikabili wenyewe kama Tanzania
ama kama Afrika. Tunahitaji wenzetu wa ukanda huu wa nchi za Kiarabu
kushirikiana nasi. Katika umoja wetu tutafanikiwa kirahisi kuliko kama
tutazikabili changamoto hizi tukiwa tumejitenga,” alisema Mheshimiwa Makamu wa
Rais.
Tanzania licha ya kuwa na wananchi wake katika nchi
mbalimbali za dunia, tawimu zinaonesha kuwa, idadi kubwa ya wananchi hao wapo
katika nchi za Kiarabu hali inayoashiria umuhimu wa kukuza mahusiano baina ya
Tanzania pekee dhidi ya ukanda wa nchi za Kiarabu. Katika siku za hivi karibuni
kupitia Diplomasia ya Uchumi, Tanzania imefungua njia kwa wawekezaji wa nchi za
Kuwait, Oman na UAE na sasa taswira ya mahusiano ya Tanzania na nchi hizi ni ya
kuvutia ambapo inatoa fursa za kunufaika kiuchumi kwa Tanzania kutoka katika
ukanda huu kuliko kwa wadau wa maendeleo wa kanda zingine ambazo Tanzania
imekuwa ikishirikiana nazo.
Akizungumza wakati wa kutoa taarifa ya kikao hiki kwa Makamu
wa Rais, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye pia yupo
katika msafara wa Mheshimiwa Makamu wa Rais, Bernard Membe alisema, kazi kubwa
ya mahusiano baina ya Tanzania na nchi za ukanda huu imejengwa na Rais Jakaya
Kikwete na sasa milango imefunguliwa kwa Watanzania kuchangamkia fursa za
maendeleo hasa katika suala zima la masoko ya bidhaa za kilimo, ufiugaji na
utalii.
Katika Hotuba yake kwenye mkutano huu, Mheshimiwa Makamu wa
Rais licha ya kutoa shukrani na salamu za Tanzania kwa Amiri wa Kuwait, Sheikh
Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah na wananchi wa Kuwait na kwa viongozi wote wan
chi za kanda hizi mbili, Mheshimiwa Makamu wa Rais alifafanua kuwa Tanzania
inatambua mahusiano ya kitamaduni, kihistoria na kijiografia yaliyopo baina ya
kanda hizi mbili na kwamba zaidi ya theluthi mbili ya watu wa ukanda wa nchi za
Kiarabu wanaishi Afrika hali inayochagiza umuhimu wa uhusiano wa kanda hizi.
Pia Mheshimiwa Makamu wa Rais alifafanua kuwa, Mkutanouliofanyika Libya mwaka
2011, haukuonesha mafanikio ya wazi hasa katika miradi ya Maendeleo na akauomba
mkutano huu wa Kuwait, kuhakikisha kanda hizi zinaongeza spidi ya kufanikisha
malengo ya kimaendeleo, ili wananchi wa kanda hizi wazidi kunufaika kutokana na
mahusiano haya.
Katika msafara huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais pia
ameambatana na Waziri wa Kilimo na Chakula, Enginia Christopher Chiza, Waziri
wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati wa SMZ, Ramadhan Shaaban, Naibu Waziri wa
Viwanda na Biashara, Gregory Teu, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Servacius
Likwelile na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Mussa. Pia katika
msafara huo wapo wabunge Hamad Rashid na Khalifa Khalifa.
Imetolewa na: Boniphace Makene
Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais






No comments:
Post a Comment