Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akiwahutubia wananchi wa mji wa Vwawa kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika jioni ya leo katika mji huo ambao ndiyo makao makuu ya
wilaya ya Mbozi, mkutano huo umehudhuriwa na wananchi mbalimbali wa
mji wa vwawa, Katika ziara hiyo Kinana ameongozana na Katibu wa NEC
Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa
NEC Siasa na Uhusiani wa Kimataifa, Akizungumza katika mkutano huo
Nape Nnauye amesema Injinia Christopher Chiza aache kuzungumza na
vyombo vya habari badala yake aandae majibu kwa ajili ya kuhojiwa
kwenye kikao cha Kamati Kuu kwa sababu kuitwa kwake kwenye kamati kuu
ya CCM hakukwepeki, Kutokana na matatizo na malalamiko ya wakulima
kuhusu pembejeo, kukopwa mazao yao na suala zima la wakulima kuikataa
mbolea ya Minjingu huku wakilazimishwa kuitumia.
Kutoka kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.
Abbas Kandoro, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Dr. Asha
Rozi Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki Mh. Godfrey
Zambi na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi wakipanda
miti katika eneo ambalo zahanati ya kijiji cha Mtunduru kata ya Isansa
inajengwa kwa ajili ya kutunza mazingira na kuzuia upepo.

Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa wilaya
ya Viwawa. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akiwa amekaa na wanachama wa CCM kijiji cha Ntunduru Kata ya
Isansa
Dr. Asha Rose Migiro akiwahutubia wanambozi
leo
Wapiganaji Ahmed Michuzi , Richard
Mwaikenda na Bashir Nkoromo wakiwa wamepumzika. 

No comments:
Post a Comment