TIMU za Taifa za Algeria, France na Ghana zimefuzu kuchezofainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa nchini Brazil mwakani.
Algeria leo usiku imekata tiketi ya kucheza Kombe la Dunia nchini Brazil 2014 na kuwa timu pekee ya kiarabu kutoka Afrika itakayoshiriki michuano hiyo mwakani.
Algeria wamefanikiwa kufuza kucheza fainali hizo baada leo usiku kuiondosha Burkina Faso katika mbio hizo baada ya kushinda wakiwa kwao bao 1-0 na kufanya matokeo ya jumla kuwa mabao 3-3, na kufanya wao kupenya na faida ya mabao ya ugenini. Mchezo wa awali Burkina Faso walishinda mabao 3-2.
Waarabu hao wametinga hatua hiyo na kuwaacha wenzao Misri iliyoondolewa na Ghana wakati Tunisia walitupwa nje na Cameroon.
Nao Frnce leo wameshinda jumla ya mabao 3-0 na kufanya kuibuka na jumla ya mabao 3-2, baada mchezo wa kwanza kupigwa mabao 2-0 na Ukraine.
TIMU ya Taifa ya Ghana pamoja na kupoteza mchezo wake wa leo usiku dhidi ya Misri kwa mabao 2-1 lakini wamefanikiwa kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014 za nchini Brazil, katika mchezo uliochezwa jijini Cairo, nchini Misri.
Ghana imefuzu hatua kwa jumla ya mabao 7-3 baada ya kushinda kwa ushindi mnono wa mchezo wa kwanza kwa mabao 6-1 mchezo uliochezwa jijini Kumasi.
Misri ambayo iliingia uwanjani ikiwa na nia ya kupata ushindi wa mabao 5-0 ili waweze kufuzu katika fainali hizo lakini walijikuta hadi wanaenda mapunziko wakiwa mbele kwa bao moja lililofungwa na Amr Zaki.

No comments:
Post a Comment