Ujenzi wa Barabara ya Morogoro na nyinginezo za jijini Dar es Salaam, unaoendelea umekuwa ukisababisha foleni kubwa za magari na hasa katika barabara hii eneo la Kimara, ambapo wafanyakazi wengi wanaishi maeneo haya huchelewa maofisini na wengine wenye usafiri binafsi wakilazimika kutumia njia ya Goba inayotokea Samaki kuelekea mwenge ama njia ya chini ya Kawe ili kukwepa foleni.
Aidha hivi sasa kutokana na magari ya daladala kutofika katika maeneo ya katikati ya mji na hasa maeneo ya Posta kutokana na upanuzi wa barabara za mabasi yaendayo kasi, wasafiri wengi wamekuwa wakitembea kwa miguu na hasa nyakati za asubuhi na jioni, ambao wengi wao huachwa Kituo cha Mnazi Mmoja na wengine kutembea hadi Kivukoni.


No comments:
Post a Comment