Habari za Punde

*WAKAZI WA KIGOMA WAITIKIA WITO NA KUFAIDIKA NA NJIA MPYA YA UANIKAJI WA DAGAA NA KUPATA DAGAA WALIO BORA

 Dagaa wa Kigoma wakiwa wameanikwa kwa kutumia njia ya kisasa baada ya wavuvi na wakazi wa Mji wa Kigoma kupewa darasa kuhusu upatikanaji wa Dagaa bora wa daraja la kwanza 'Grade one'.Awali wakzi na wavuvi wa mkoa huo walikuwa wakianika dagaa chini ardhini jambo ambalo lilikuwa likisababisha dagaa hao kuwa na rangi ya udongo na kujaa mchanga, lakini tangu walipopatiwa semina kuhusu njia hiyo, wakazi walio wengi wameitikia wito na kuitumia njia hiyo na kuona mafaniki oyake.  
Dagaa hawa ambao huanika kwa njia hii, huuzwa kwa Sh. 15, 000 hadi 13,000,wakati wale wengine wanaoanikwa kawaida huuzwa kwa sh. 9,000 hadi 7,000/=.
Hapa ni katika moja ya eneo linalopatikana dagaa hawa kwa wingi, katika kivuko cha Kibilizi mjini Kigoma.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.