Habari za Punde

*HOYCE TEMU, LULU MUSSA, WALAMBA NONDOZZZ YA SHAHADA YA UZAMILI YA MAWASILIANO YA UMMA

Picture 018
Miss Tanzania wa 1999, ambaye pia ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu akipozi mara baada ya kulamba Nondozzz ya shahada ya Uzamili wa Mawasiliano ya Umma katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine jijini Mwanza.
Kulia ni  Mdau wa tasnia ya habari nchini.
Picture 013
Hoyce Temu katika pozi na marafiki zake mara baada ya kulamba Nondozz.
Picture 026
Lulu Musa, Afisa Uhusiano wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira kwa kulamba Nondozz ya shahada ya Uzamili wa Mawasiliano ya Umma katika chuo cha St. Augustine University kwenye mahafali ya 15 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa Juma.
Picture 045
Mbali na kula Nondozz kwenye siku hiyo maalum Hoyce Temu ambaye pia ni Mtangazaji wa Kipindi cha Mimi na Tanzania aliamua kufanya mahojiano na baadhi ya wahitimu kwa ajili ya kipindi chake.
Picture 055
Mlimbwende Hoyce Temu akizungumza na mwandishi wa habari wa ITV kuhusiana na taalum aliyoipata itakavyoweza kuboresha utendaji wake kazini pamoja na kuendelea kuisaidia jamii inayomzunguka kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania.
Picture 070
Mwanandishi wa habari wa kituo cha ITV Shaban Tole akimpongeza Hoyce Temu.
Picture 078
Hoyce Temu katika picha ya kumbukumbu na marafiki.
Picture 071
Hoyce Temu akiondoka eneo la tukio na furaha isiyo na kifani.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.