Marehemu Nelson Rolihlahla Mandela enzi za uhai wake.
Habari zilizoufikia mtandao huu zinaripoti kuwa, Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amefariki dunia majira ya saa mbili za usiku wa jana na ripoti kamili ya kifi chake zikatolewa rasmi usiku wa saa nane. Mandera amefariki dunia jijini Johannesburg, Afrika Kusini akiwa na umri wa miaka 95 . Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma amethibitisha taarifa hizo!
Rais Zuma amesema "taifa limepoteza mtu muhimu" na kuongeza "kwa sasa amepumzika. Yupo mahala pema"
Mzee Mandela aliyekuwa akisumbuliwa na homa ya mapafu amefariki akiwa amezungukwa na familia yake nyumbani kwake Johannesburg.
Mandela atazikwa kitaifa na bendera zitapepea nusu mlingoti, alisema Rais Zuma.
Alikuwa akipatiwa matibabu kwa takribani miaka mitatu iliyopita na hali yake ilibadilika zaidi katika miezi sita ya mwisho kabla ya kifo chake.
Mpiganaji huyo wa ubaguzi wa rangi, aliingia Ikulu ya Afrika Kusini akiwa mtu mweusi wa kwanza kuiongoza nchi hiyo mwaka 1994 mpaka 1999 baada ya kutumikia kifungo cha miaka 27 gerezani.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema: "taa kubwa imezimika duniani
"Nelson Mandela alikuwa shujaa"
"Nelson Mandela alikuwa shujaa"
********************************************
THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
Fax: 255-22-2113425
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia kwake, kwa mkewe Bi. Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu". Ameongeza Rais Kikwete.
Rais amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomuwezesha kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.
"Mandela ni mfano bora kwa wanadamu wa jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa . Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kwa jumla kuiga mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na wananchi wenzake" .Rais ameongeza kusema, "Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela mahali pema peponi".
Kufuatia kifo hicho Rais ametangaza siku 3 za maombolezo kuanzia leo tarehe 6 hadi 8 Disemba, 2013.
Aidha, Mheshimiwa Rais ameagiza kuwa katika siku hizo 3 bendera zote zipepee nusu mlingoti.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu,
DAR AS SALAAM.
06 Desemba,2013

No comments:
Post a Comment