Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti kwa niaba ya TBC Mtangazaji mahiri wa stesheni hiyo ya Taifa Bi. Amina Mollel katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam jana Novemba 3, 2013 wakati wa sherehe za Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Amina Morel baada ya kumkabidhi cheti.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi alipowasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Bw. Amon Anastaz akisoma risala kwa kutumia braille katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani.
Mkalimani wa lugha ya viziwi, akiendelea kutafsiri wakati wa risala.....
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIRYAWATA) akiwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi pamoja na Mwenyekiti wa (SHIVWATA) baada ya kuhutubia katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa cheti kwa Bw. Frederick Msigallah wa CCBRT katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani
PICHA NA IKULU








No comments:
Post a Comment