Habari za Punde

*SAMATTA USO KWA USO NA OKWI ROBO FAINALI ZA CHALENJI,

BAO pekee la mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, anayecheza soka la kulipwa na Klabu ya TP Mzembe, Mbwana Samatta, limeiwezesha timu ta Taifa 'Kilimanjaro Stars', kutinga hatua ya Robo fainali katika michuani ya Chalenji, inayoendelea nchini Kenya, baada ya leo kuibanjua Burundi kwa bao 1-0.


Bao pekee la Stars leo limefungwa na Mbwana Samatta kwa kichwa dakika ya saba ya mchezo huo, akiunganisha krosi maridadi ya mshambuliaji mwenzake wa TP Mazembe ya DRC, Thomas Ulimwengu.
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Stars, Mbwana Samatta, akimtoka beki wa Burundi wakati w amchezo uliochezwa leo Nakuru Kenya. Picha na kwa hisani ya Bin Zubeiry
************************************
Kwa matokeo hayo sasa Stars iliyo chini ya Kocha Mdenmark, Kim Poulsen imemaliza hatu ya makundi ikiwa na pointi saba, baada ya awali kushinda 1-0 dhidi ya Somalia na kutoa sare ya bila kufungana na Zambia.

Hadi sasa, Tanzania Bara na Zambia zinalingana kwa kila kitu na iwapo Chipolopolo itaifunga zaidi ya mabao mawili Somalia, ndiyo itaongoza Kundi na maana yake sasa, Stars itakutana na mabingwa watetezi, Uganda, The Cranes katika Robo Fainali.  

Iwapo Stars itakutana na The Cranes yenye wachezaji nyota kama Emmanuel Okwi aliyewahi kuchezea Simba na Hamisi Kiiza anayechezea Yanga za Dar es Salaam, itakuwa nafasi nzuri kwao kulipa kisasi cha kufungwa 3-0 za mwaka jana katika Nusu Fainali mjini Kampala, Uganda. 

Lakini kama Stars itaongoza Kundi B, itakutana na Rwanda inayoongozwa na Nahodha, Haruna Niyonzima wa Yanga SC ya Dar es Salaam.  

Tanzania Bara; Ivo Mapunda, Himid Mao, Erasto Nyoni, Said Morad, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Amri Kiemba/Haroun Chanongo dk77, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Mrisho Ngassa/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk81. 

Burundi; Arakaza Arthur, Hakizimana Hassan/Abdulrazack Fiston dk81, Hererimana Rashid, Hakizimana Issa, Nsabiyumva Frederic, Nduwimana Jean, Ndikumana Yussuf, Duhayinavyi Gael/Mussa Mosi, Nduwarugira Christophe, Habonimana Celestin na Hussein Shaaban/Ndarusanze Claude. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.