Habari za Punde

*ZANZNIBAR HEROES 'OUT' MICHUANO YA CHALENJI

Beki wa Kenya, Joackins Atudo akilala kudokoa mpira miguuni mwa kiungo wa Zanzibar, Sabri Ali Makame wakati wa mchezo wa Kombe la Challenge kwenye Uwanja wa Afrah, Nakuru.
Mabao ya Harambee yalifungwa na beki wa Azam FC ya Dar es Salaam, Joackins Atudo kwa penalti dakika ya sita na mshambuliaji wa AFC Leopards ya Kenya, Allan Wanga dakika ya 60.



Kwa ushindi huo, Kenya imetimiza pointi saba baada ya awali kuifunga Sudan Kusini 3-1 na kutoa sare ya bila kufungana na Ethiopia.

Zanzibar ambayo sasa inabaki na pointi zake tatu, itasubiri mustakabali wake wa kwenda Robo Fainali katika nafasi mbili za best losers.

Rwanda ambayo haina pointi hadi sasa inaweza kuungana na timu moja ya kundi B pamoja na Zanzibar kuwania kufuzu katika nafasi za best losers, iwapo itaifunga Eritrea katika mchezo wake wa mwisho. 

Zambia, Tanzania Bara na Burundi timu mbili kati ya hizo zitafuzu moja kwa moja baada ya matokeo ya mechi za mwisho leo na moja itaingia kwenye kapu la best losers.
Kundi C Uganda na Sudan tayari zimefuzu na Rwanda na Eritrea zitawania nafasi ya best losers. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.