Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki, akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni.
******************************************
Na Sufianimafoto, Reporter, Dar
MKURUGENZI wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choki, ametangaza rasmi
kuwatimua kazi wasanii wake watatu walioshiriki onyesho la Usiku wa Mwana Dar
es Salaam, lililoandaliwa na Bendi Hasimu wake ya Twanga Pepeta.
Akizungumza na Sufianimafoto kwa njia ya simu, Chocki, alisema kuwa
kamwe hawezi kuyumbishwa na wafanyakazi wake mweneye na kuongeza kuwa msimamo
wake wa kuwatimua wasanii hao upo pale pale kutokana na wao kujifukuzisha kazi wenyewe
kwa kukiuka taratibu na sheria ya bendi hiyo.
Pamoja na kwamba nimefanyanao kazi kwa muda mrefu miongoni mwa hao
lakini inabidi waheshimu taratibu na agizo la uongozi.
“Mmoja wao tayari ameleta barua ya kuomba msamaha lakini hiyo bado
haisaidii, kwani tayari alishaonyesha dharau kwa kutenda kosa wakati akifahamu
kuwa ni kosa na akihisi kukutwa na suala hili’’. Alisema Choki
Wasanii hao walioshiriki
Usiku wa Mwana Dar es Salaam uliofanyika katika ukumbi wa Mango Garden
Kinondoni, Jumamosi iliyopita, ni Danger Boy, Sabrina na Maria Soloma.
‘’Miongoni mwao yupo mmoja ambaye
amekuwa akitangaza kuwa Extra Bongo haina maslahi ya kutosha, na cha kushangaza
zaidi yeye ndiye amekuwa wa kwanza kuandika barua ya kuomba msamaha’’. Alisema Choki
Ally Chocky amewataka wasanii na
viongozi wa bendi wasitumie kigezo cha kutolipwa mshahara kama fimbo ya kuvunja
taratibu na sheria za bendi hiyo.
Ally Chocky amewataka wasanii na
viongozi wa bendi wasitumie kigezo cha kutolipwa mshahara kama fimbo ya kuvunja
taratibu na sheria za bendi hiyo.
“Sidhani kama kuna bendi hata moja
inayofanya mambo yake kwa asilimia mia moja, ila zote ni sawa tu tunabadilisha
mazingira tu, kwani najua hapa hapa Bongo pia zipi baadhi ya bendi ambazo
zimeshindwa kabisa kulipa mishahara kwa wafanyakazi wake na badala yake
zimekuwa zikifanya kazi na kulipana posho tu, “Ugumu
wa bishara ya muziki wa dansi unajulikana, bendi nyingi zinashindwa kujiendesha
kwa kipato kinachopatikana ukumbini, hivyo wakati mwingine suala la kuchelewa
kwa mishahara halikwepeki, Kwa upande wangu naamini kuwa Tamasha hilo,
liliandaliwa rasmi kwa ajili kuzalisha migogoro
baina ya wamiliki wa bendi na wasanii ili watu wajizolee wasanii wa bure pale
watakapotimuliwa na bendi zao na mimi nifanya hivyo ili wawachukue wasanii
wanaowahitaji, kisha nitazalishwa wengine. ’’. alisema Chocki


No comments:
Post a Comment