Habari za Punde

*KABURI LA GWIJI LA MUZIKI MBARAKA MWINSHEHE MAFICHONI MZENGA, JOHN KOMBA UNAKUMBUKA KABURI HILI???

 Wiki iliyopita kamera ya sufianimafoto, ilifanikiwa kutinga katika Kijiji cha Mzenga na kutembelea katika Pori lililopo kijijini hapo alikozikwa Gwiji la Muziki Mbaraka Mwaruka Mwinshehe na kukuta likiwa katika hali kama hii. 

Mkazi wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Khalfan Mzuika au Mzee Nyoka, almaaruf kama 'Jambo Nyama', alisema kuwa kaburi hilo lilijengewa na Kiongozi wa Kundi la muziki la TOT Plus, Kaptain John Komba, aliyewahi kufika eneo hilo akiwa na kundi zima la TOT wakiwa na usafiri wa Roli lililokuwa likitumiwa na bendi hiyo kama Jukwaa na kuomba kuonyeshwa kaburi hilo na kisha kulijengea na kuwa katika hali kama hii hadi leo. 
Pichani ni Mzee Nyoka au kwa jina maarufu la Jeshini 'Jambo Nyama, kama alivyokuwa akitambulika na wanafunzi wake kama John Komba na wengineo enzi hizo wakati wakiwa Jeshini alipowapokea na kuwarukisha kichura. Hapa alikuwa akimtembeza Mafoto katika makaburi hayo ambayo pia wapo nduguze na Mwinshehe pamoja na wazazi wao. 

4 comments:

  1. jamani kwanini kaburi lipo katika mazingira hayo??mzee mwinshehe ni mtu maarufu sana

    ReplyDelete
  2. tumuenzi mwanamuziki wetu maarufu

    ReplyDelete
  3. kweli nimeamini binadamu unathaminika ukiwa hai,je selikali kwanini hawathamini mchango wa hayati mbaraka mwinshehe??

    ReplyDelete
  4. nawaomba wadau wenye mapenzi mema tujitolee kulijengea kaburi la mbaraka mwinshehe

    ReplyDelete

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.