Habari za Punde

*MATOKEO YA AWALI UCHAGUZI WA SIMBA, AVEVA MWENYEKITI, KABURU MAKAMU WAKE, WAJUMBE BADO MATOKEO

 Mgombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu wa Simba, Evans Aveva (katikati) na Swed Nkwabi (kushoto), wakiangalia muda kwa pamoja baada ya kupiga kura zao katika uchaguzi huo, wakisubiri matokeo na kutangazwa kwa washindi katika uchaguzi huo uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Bwalo la Poilisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Evans Aveva na mpinzani wake, Tupa, wakipiga kura.
Katika uchaguzi huo matokeo ya awali yalikuwa yakionyesha kuwa, Evans Elieza Aveva, alikuwa akiongoza kwa kujizolea jumla ya kura 1452 kati ya 1845  zilizopigwa na kutoa matumaini kwa wapiga kura wake ya kuibuka kidedea katika uchaguzi huo.

Mpinzani wake Andrew Tupa, hadi tunakwenda mitamboni alikuwa amejinyakulia jumla ya kura 387 wakati kura sita zimeharibika. Hata hivyo, matokeo rasmi ya uchaguzi huo yatatangazwa na Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo chini ya Mwenyekiti Dk Damas Ndumbaro baadaye.

Wakati huo huo, Geoffrey Nyange 'Kaburu' (pichani akipiga kura) ameshinda nafasi ya Umakamu wa Rais wa Klabu hiyo ya Simba SC baada ya kupata jumla ya kura 1043 akimshinda mpinzani wake wa karibu Jamhuri Mussa Kihwelo 'Julio' aliyepata kura 413 na Swedi Nkwabi kura 300. Hata hivyo, hizo ni taarifa za awali, matokeo kamili yatatangazwa na Kamati ya Uchaguzi baadaye.
 Julio akipiga kura..
 Mwanachama wa Simba, 'Madenge' akipiga kura
 Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali, akipiga kura.
 Aliyekuwa msemaji wa Simba Asha Mhaji, akipiga kura 
 Mmoja kati ya wagombea wa nafasi ya Ujumbe, Ibrahim Masoud (kulia) akipozi wakati akisubiri matokeo baada ya kupiga kura.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakipiga kazi wakiwa humo humo ukumbini.
 Mwenyekiti wa Simba aliyemaliza muda wake, Aden Ismail Rage, akitimka eneo hilo mida ya mchana, baada ya kupiga kura.
 Baadhi ya wanachama wa Simba wakifuatilia kila linaloendelea ukumbini hapo.
 Wengine walichoka na kuanza kuuchapa usingizi kwa kuchelewa kupata matokeo.
Baadhi ya wanachama wakifuatilia kwa makini.....

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.