Habari za Punde

*PINDA AHUDHURIA MKUTANO WA BENKI YA DUNIA

Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda akizungumza na waandishi wa habari  nje ya Hotel ya Serena ambapo alihudhuria Mkutano wa Tano unaohusu masuala ya Uchumi,kulia kwake ni mkurugenzi wa benki ya Dunia nchini Ndugu Philippe Dongier.
 Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Philippe Dongier akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa kivukoni Serena Hotel jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na Mwandishi wa Mada Ndugu Jacques Morisset ambapo aliwaeleza waandishi hao Tanzania ina nafasi kubwa ya kupanua wigo wa ajira kwa kutengeneza mazingira ya kufanyia kazi yenye ubora hasa kwenye  miji inayokuwa kwa kasi hii itasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa Vijana na Wanawake.
 Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Philippe Dongier akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa kivukoni Serena Hotel jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na Mwandishi wa Mada Ndugu Jacques Morisset ambapo alikiri pamoja na kukua kwa uchumi lakini bado uchumi haujafungua au kutengeneza ajira kwa wananchi . Picha na Adam Mzee 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.