Ndugu Wanajumuiya,
Kufuatia maombi kutoka kwa Wanajumuiya wenzetu wanaofunga mwezi Mtukufu wa Ramadhani (ambao ni mwezi ujao) na hivyo watakuwa na swaumu kipindi hicho, wametuomba tusogeze kikao chetu cha Jumuiya kilichokuwa kifanyike tarehe 5 Julai 2014 hadi tarehe 2 Agosti 2014.
Kwa heshima ya ndugu zetu wanaofunga Mwezi wa Ramadhani kikao kitafanyika tarehe 2 Agosti 2014, kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi au kumi na mbili jioni. Nawaomba wote mkumbuke tarehe hii na “please, save this date for our community meeting”.
Tumeomba kikao kifanyike Mount Vernon, kwenye uwanja wa ubalozi pale pale tulipofanyia uchaguzi mwaka jana. Kama sehemu hii isipopatikana basi tutatafuta sehemu nyingine kule Mount Vernon.
Sababu ya kuomba kufanyikia Mount Vernon ni kuwa tumekuwa tuki "rotate" sherehe, matukio na vikao vilivyopita vilifanyika Manhattan, Brooklyn, Roosevelt Island na Queens. Na sasa itakuwa vizuri wenzetu wa Mount Vernon nao wawe wenyeji wa kikao hiki.
Sababu ya kufanyika kikao zipo kwenye email niliyowatumia juma lililopita.
Ukipata taarifa hizi tunaomba umwambie mwenzako. Na nawaomba wote mje kwa wingi tarehe 2 Agosti 2014 kwenye mkutano wa Jumuiya yenu.
Asanteni.
Katibu,
Deogratius Mhella.
New York Tanzanian Community
No comments:
Post a Comment