Taarifa kwa vyombo vya habari
Imetolewa
leo tarehe 16 Julai 2014
Na
Dismas Lyassa
Mgombea Urais wa TUCTA; Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi
Mgombea Urais wa TUCTA; Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi
Salaam
Wapendwa ndugu zangu wana
habari…Asalam Aleikum…Tumsifu Yesu Kristo… Bwana Yesu Asifiwe…!
Shukrani
Ndugu wanahabari
Nawapenda kuwashukuru kwa
ujio wenu. Nichukue fursa hii niwatambulishe walioko mbele yenu ili
kufahamiana. Nianze kwa kujitambulisha mimi mwenyewe, naitwa Dismas Lyassa, ni
mwandishi wa habari mwenzenu…nimekuwa katika hii kazi kwa miaka 20 sasa na
nimewahi kufanyia kazi katika magazeti mbalimbali yakiwamo Alasiri, Financial
Times, Leo ni Leo na tangu 2005 nimekuwa nikifanyia kazi katika gazeti la
Mwananchi hadi sasa nikiwa mhariri anayeshughulikia masuala ya biashara na
uchumi. Pia toka mwaka 2012 nilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa COTWU tawi la
Mwananchi Communications Limited, nafasi ambayo kisheria mtu anapaswa kudumu
kwa miaka mitano, lakini akitaka anaweza kugombea.
Utambulisho
Ndugu wanahabari
Wengine niliombatana nao ni
mke wangu Mchungaji Rightess Lyassa wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Kawe -Dar es
Salaam, Mussa Mwakalinga Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na
Usafirishaji (COTWU) kanda ya Dar es Salaam, wakili wangu Jebra Kambole kutoka
kampuni ya Uwakili ya Law Guards ya Jijini Dar es Salaam, na meneja kampeni
Khamis Tembo.
Ndugu wanahabari
Lengo hasa la kuwaiteni
mahali hapa ni kutoa taarifa kwenu kuwa ninagombea Urais wa Shirikisho la vyama
vya wafanyakazi Tanzania, uchaguzi ambao unatarajiwa kufanyika Agosti 4-5,
Dodoma.
Vipaumbele vyangu ni vyangu
Ndugu wanahabari
Nina malengo ya kuifufua na
kuleta TUCTA yenye uhai na mabadiliko ya kweli kwa kufanya yafuatayo;
Ndugu wanahabari
1. Kupigania na kulinda haki za wafanyakazi;
Katika kipaumbele hili lengo
hasa ni kuondoa matatizo sugu ya wafanyakazi yakiwamo-:
i.
Kulipwa ujira/mishahara duni isiyoendana na uhalisia wa
maisha.
ii.
Ucheleweshaji wa upatikanaji wa ujira/mishahara
iii.
Ucheleweshaji fedha za kujikimu kwa waajiriwa wapya/
kiwango kidogo cha fedha za kujikimu
iv.
Uhaba au kutokuwepo kabisa makazi kwa wafanyakazi wapya
v.
Rushwa na kuajiri kwa misingi ya kujuana kwa mfano katika
Halmashauri ya Siha, wilaya ambayo imegawanywa kutoka Hai, kuna pori kubwa la
West Kilimanjaro mlimani kabisa, hakuna maendeleo…ni suala la kawaida kuona
watu wakiongea kilugha ofisini kama lugha ya Taifa
vi.
Wakubwa yaani mabosi kujifanya Mungu kwa kuwaendesha
wafanyakazi kwa kadri wanavyotaka wao, sivyo inavyosema sheria.
vii.
Uwepo wa mpangilio usio sawa wa ujira/mishahara.
viii.
Kutopewa posho au kupewa kidogo au kutopewa kwa wakati
ix.
Fedha za uhamisho na likizo; kwa mfano kuna walimu ambao
wameanza kazi 2004 NIT Shule ya msingi Dar es Salaam wamelipwa fedha za likizo
mara moja mwaka 2012, mfano halisi ni mwalimu Ruth Natumwa, huyo ni kati ya
walimu hao. Matatizo ya walimu kimsingi ni janga la taifa, yapo Taifa zima, kwa
mfano katika shule ya Sekondari Kizota, Dodoma kuna walimu wengi wana madai yao dhidi ya Serikali, waliajiriwa
mwaka jana Machi, wakaanza kupata mshahara mwenzi wa tisa…walilipwa mshahara wa
mwezi wa tisa tu na kuendelea, ile
mingine wanaendelea kudai.
x.
Mazingira magumu ya kazi mijini na vijijini
(tunapozungumzia mazingira magumu inahusisha kutokuwepo vitendea kazi au kuwa
vichache, miundo mbinu duni nk).
xi.
Waajiri
kutochangia mifuko ya jamii
xii.
Fedha
za makato ya wafanyakazi kupitia mifuko ya jamii zimekuwa zikikopeshwa watu
wengine wasio wanachama wakiwamo wanasiasa huku wafanyakazi wenyewe wakiendelea
kuwa na maisha duni
xiii. Kufanya kazi kama kibarua kwa
miaka mingi jambo ambalo ni tofauti za sheria za kazi
xiv. Huduma za kifedha kuwa mbali na
maeneo ya kazi, hali inayosababisha wafanyakazi kutumia fedha nyingi kufuatilia
mishahara kwa vile ni mbali na eneo wanalofanyia kazi.
xv.
Kutokuwa
na mfumo unaoeleweka wa upandishaji vyeo na ujira/malipo kwa
wafanyakazi/vibarua
xvi. Waajiri hasa binafsi kufukuza
wafanyakazi hovyo/no job security…kufanya kazi bila mikataba
xvii.
Kupambana na tatizo la kodi kubwa kwa mishahara (PAYE)
xviii.
Tatizo la mabosi kutoa upendeleo wa wazi kwa baadhi ya
wafanyazi kwa sababu zisizo za kitaalamu; wakati mwingine ni kwa sababu ya
ngono; kuwataka kimapenzi wafanyakazi ili waendelee kuwepo kazini au
kupandishwa vyeo…tatizo hili linaonekana kuwa sugu, wanawake wengi maofisini
hawako huru sana, wamekuwa wakitakwa kimapenzi mno na mabosi wao, wengi
wanashindwa kujizuia, tunataka kuona kunakuwa na sheria kali dhidi ya mabosi wa
aina hii kama ilivyo katika nchi nyingine.
Ndugu wanahabari
Tatizo la ajira kuporwa na wageni
Ingawa sheria/sera za ajira zinaeleza wazi
kwamba hairuhusiwi wageni kuingia nchini zaidi ya watano kwa kazi ziziso na
ujuzi, baadhi ya makampuni yamekuwa yakiingiza wageni kwa kazi ambazo
Watanzania wengi wanaweza kuzifanya.
Ndugu wanahabari
Nitahakikisha wazawa wanapewa fursa ya
kufanya kazi nchini; hii ni pamoja na kuomba CV za wageni ili tuone kama ni
kweli hakuna Watanzania wenye sifa za kufanya hiyo kazi hiyo.
-: Kumekuwa na taarifa za uwepo wageni
katika makampuni kadhaa yakiwamo mahoteli, migodi, viwanda vya sarufi nk ambao
baadhi wanalipwa malipo makubwa tofauti na wazawa japo hawana elimu au ujuzi wa
kuwazidi wazawa. Nitakuwa na kamati maalumu ya kufuatilia waajiriwa wote
Tanzania hasa wageni ili kujua kama wanazo sifa za kufanya kazi au wanapora
nafasi za Watanzania.
Ndugu wanahabari
Nitapigania kuhakikisha tabia ya waajiri kulazimisha
waajiriwa lazima wawe na uzoefu mkubwa inapungua au kukoma kabisa
Kigezo cha kupata ajira kiwe ni uwezo wa mtu
wakati huo baada ya kufanyiwa usaili, siyo lazima awe na uzoefu wa miaka mitatu au mitano kama ambavyo
waajiri wengi wanalazimisha; tunahitaji kuona Serikali inasimamia hili. Kama
hali ni hii, wahitimu wanawezaje kupata ajira? Ni suala ambalo nitakuwa mkali
nalo mno kwa sababu lina athari kubwa kwa jamii ya Tanzania, limekuwa ni sababu
ya rushwa ikiwamo ya ngono…walioko vyuoni wengi hawana uhakika wa ajira, kwa
sababu ya tabia hii. Ni lazima tubadilike, watu waajiriwe kulingana na uwezo
wao wa kazi, siyo uzoefu.
Ndugu wanahabari
Wanafunzi shule ya Msingi/Sekondari nk wapatiwe elimu ya
kujiajiri.
Kwa nafasi nitakayokuwanayo nitaishawishi Serikali
iingize elimu ya ufundi/utengenezaji bidhaa na ujasiriamali kama mojawapo ya
masomo ya ziada kama njia ya kupambana na tatizo la ajira ambalo linaonekana
kukua nchini. Kama ambavyo kumekuwa na masomo ya dini katika shule zenu, tuwe
pia na masomo ya ujasiriamali. Nitaangalia namna ya kuzishawishi taasisi
zingine za ndani na nje kuhakikisha hili linafanyika; lengo ni kuhakikisha hata
mhitimu wa msingi au sekondari nk awe ana uwezo wa kufanya ujuzi anaotaka kama
kujenga, kushona, kufuma, kufuga, kutengeneza batiki, vikoi, sabuni, mishumaa
nk.
Ndugu wanahabari
Nitaanzisha idara mbili mpya na kuboresha zilizoko;
i.
Idara ya walemavu
Hii itahusika kuangalia hali ya maisha ya wafanyakazi walemavu nchini ikiwamo
kuwasaidia kupata baiskeli na huduma zingine muhimu.Nitatumia uzoefu wangu kwa
kushirikiana na rafiki zangu wa nje kuhakikisha hili linafanikiwa. Tutaangalia
namna ya kushirikiana na mashirika mbalimbali yakiwamo Free Wheelchair
Foundation www.wheelchairfoundation.org.
Ndugu wanahabari
Kutakuwa ni mikakati
mbalimbali kuhusu wafanyakazi walemavu na wale wanaopata ulemavu wakiwa kazini,
kwa mfano Mwenyekiti wa Wasioona mkoani Tanga amekuwa ni mtu ambaye ameumia
kazini, lakini aliishia kulipwa Sh150,000 na bandari ambako alikuwa anafanya
kazi kama kibarua. Kitendo kitakuwa na
jukumu la kufuatilia kwa ukaribu hali za wafanyakazi walemavu, kuangalia kama
wanavyotoka vyuoni wanapewa ajira au wanaishia kunyanyapaliwa? Utafiti
unaonyesha kuna wanafunzi wengi wanaohitimu masomo wakiwa na ulemavu, hata
hivyo hawaonekani kwenye maofisi wakifanya kazi. Wanakwenda wapi? Litakuwa ni
jukumu la hicho kitengo.
Ndugu wanahabari,
Idara ya pili
ni
Idara ya fursa/Career Development Department na Mafunzo
Nimetembea katika nchi tofauti Duniani ikiwemo
Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Mauritius, India, Thailand, Sweden na
Marekani…nimeona fursa kadhaa ambazo zimenishawishi kuanzisha idara maalum ya
kusaidia wafanyakazi kufahamu fursa zinazoendelea Duniani na hapa nchini. Fursa
hizo zitakuwa zinapatikana katika tovuti za TUCTA na ofisi za vyama vya
wafanyakazi mikoani. Baadhi ya fursa ni namna gani mtu anaweza kusoma nje ya
nchi bila kulipa ada kwa kozi za muda mrefu na mfupi, fursa ya mashirika ambayo
yanatoa misaada kwenye sekta mbalimbali.
-Kwa mfano kuna mashirika
kama www.nuffic.nl
au vyuo ambavyo mtu anaweza kusoma bure bila kulipa chembe ya ada kama www.berea.edu ya Marekani na fursa nyingine nyingi.
Nimegundua Watanzania wengi hawanufaiki sana na fursa hizi. Ziko pia taasisi
nyingine zinatoa.
Ndugu wanahabari
Idara hii itakuwa na majukumu
ya kutoa elimu kwa wafanyakazi kuzifahamu sheria za kazi, hali kadhalika
itakuwa inawasiliana na waajiri ili zaidi ya barua ya ajira au mkataba wanaompa
mwajiriwa, ampe pia na chapisho letu
ambalo mwajiriwa anapaswa kupewa siku ya kuajiriwa kwake ili ajue kwa uhakika
sheria za kazi zinasemaje; haki ya mwajiriwa kwa mwajiri au ipi na haki ya
mwajiri kwa mwajiriwa ni ipi; tutashawishi hili liwe ni suala la lazima.
Tutakuwa na vituo maalum vya msaada wa kisheria mikoani kote au kwenye kanda.
Tutakuwa na vipindi kwenye televisheni angalau kila mwezi mara kuelezea masuala
ya sheria za kazi. Tutaitumia tovuti ya TUCTA
kuwa ya kisasa zaidi.
Ndugu wanahabari
Kulifufua gazeti
la Mfanyakazi ndani ya siku 90 ili liwe sauti thabiti ya wafanyakazi
Haijalishi kama TUCTA itakuwa
na fedha au la, nitahakikisha ndani ya siku 126
litakuwa mitaani likiandika habari mbalimbali hasa likitumika kama sauti
ya wafanyakazi na yote ambayo yataonekana ni ya maana kwa ustawi wa taifa. Nina
uzoefu zaidi ya miaka 20 katika sekya ya habari kama Mhariri, na hata sasa ni
Mhariri wa Biashara gazeti la Mwananchi, nitahakikisha tunatafuta fedha ndani
na nje ya TUCTA ikiwamo kuwatumia wafanyabiashara kwa kubadilishana msaada kwa
matangazo kwa muda, ili hatimaye liweze kuwa mitaani. Ni aibu kubwa kuona nchi
ina wafanyakazi wengi, lakini gazeti kama hili la wafanyakazi haliko mitaani.
Ndugu wanahabari
Kuimarisha
uhusiano wa vyama vya ndani na vyama vya nje
Nitahakikisha nafanya
mawasiliano na mashirika mengine yakiwamo International Trade Union
Confederation, Secretary General Sharan
Barrow na mashirika mengine ili kuona namna gani vyama vya wafanyakazi
vya nchini vinanufaika na ushirikiano huo kwa kubadilishana uzoefu na kadhalika
mara kwa mara kadri inavyowezekana.
Ndugu wanahabari
Nitatutumia uzoefu wangu wa
shughuli za kuwasiliana na vyuo vya nje na uzoefu wangu wa kufanya kazi katika
mashirika mbalimbali ya nje kama muwakilishi wao hapa nchini, na kutembea nchi mbalimbali, kuviunganisha vyama
vya ndani vya wafanyakazi, kuwa na ukaribu zaidi na vile vya nje, na pia
kujenga uwezekano wa viongozi nchini kwenda nje kupitia ushirikiano huo.
Ndugu wanahabari
Hili linawezekana kwa njia mbili, kwanza kama washirika
wetu kwa vile tutakuwa tuna mawasiliano ya karibu na aina ya chama ambacho mtu
anatoka, kwa mfano kama COTWU, TTU, TALGWU, TUICO, TAMICO, TEWUTA, DOWUTA,
TPAWU, RAAWU, TUGHE, CHODAWU, TRAWU. Nahitaji kuona ofisi za vyama vya
wafanyakazi nchini zinakuwa za kuvutia kwa kuzipatia vitendea kazi, kuna
mashirika nayafahamu, tunaweza kuyatumia kuwasiliana nayo yakatusaidia kama
vile Computer Aid International la Uingereza ambalo hutoa misaada ya computer
za aina mbalimbali kwa nchi maskini kama Tanzania (www.computeraid.org). Nje ya
hiyo nitakuwa na vikao na viongozi wa chama kimoja badala ya kingine kuangalia
namna gani tunaweza kuboresha shughuli za utendaji za ndani na nje hasa kuimarisha
rasilimali watu na vifaa. Lengo kubwa la kuomba niwe Rais wa TUCTA ni kuangalia
namna gani tunaweza kushirikiana na wafanyakazi na viongozi wa vyama katika
kuimarisha wafanyakazi, kwani malalamiko ni mengi. Tutaendeleza
mali za TUCTA zikiwamo Chuo cha Wafanyakazi Mbeya na maeneo mengine.
Ndugu wanahabari
NAMNA GANI HAYA YATAWEZEKANA?
Mkakati wa kuondoa kero zote
zilizoelezwa juu utafanikiwa kwa majadiliano yenye ukomo (deadline) na
Serikali/waajiri, au kufanya chochote ambacho katiba inaruhusu. Sheria ziko
wazi, nitahamasisha zifuatwe na zifahamike. Shida kubwa ninayoiona kwa sasa,
wafanyakazi wengi hawajui haki zao pia msaada wa vyama katika kuwasaidia
wafanyakazi ni mdogo.
Ndugu wanahabari
Hata hivyo mkakati hasa ni
kuangalia TUCTA kwa kushirikiana na vyama shiriki vinafanya nini kuondoa
changamoto ambazo sisi wenyewe tunaweza kuziondoa. Uongozi siyo kulalamika,
bali kuthubutu kuchukua hatua zinazoweza kuondoa shida zilizoko. Tayari
nimeanza kuwasiliana na vyama mbalimbali vya wafanyakazi katika mataifa ya nje
ili kuangalia namna gani tunashirikiana kwa maana ya kubadilishana uzoefu nk.
Ndugu wanahabari
Ofisi nyingi za vyama vya
wafanyakazi zimechakaa, naangalia uwezekano wa kushirikiana nao katika hili kwa
njia ya kutafuta wafadhili wa nje au kubuni miradi itakayosaidia kuondoa hali
hiyo; nataka pia maisha ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi kwa
ujumla yabadilike kwa kutumia jitihada hizo nilizozieleza juu, nafahamu vizuri
namna ya kusaka wafadhili, kwani ni shughuli ambayo nimekuwa nikifanya kwa muda
mrefu kupitia taasisi yangu ya Global Source Watch, niliyoianzisha toka mwaka
2001 ambayo imekuwa ikifanya kazi ya kuwaunganisha watu na vyuo zaidi ya 78 vya
nje kama Marekani, Canada, Greece, India, Malaysia nk.
Ndugu wanahabari
Nafahamu kuna vyama vina
miradi ya maendeleo, vinawasaidiaje wanachama wao? Nahitaji niwe Rais ili
nishirikiane na vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi kwa ujumla kuleta tija kwa
Watanzania. Tusiwe watu wa kunyoosheana vidole…kila mtu awe chanzo cha mabadiliko
anayotaka kuyaona Tanzania! Naamini kila mtu akifanya kazi zake vizuri…Tanzania
itakuwa na maendeleo kwa kasi. Wafanyakazi wanahitaji mambo mengi zaidi ya
kuhamasishwa migomo, lakini kama tutaamua kugoma, tunapaswa kugoma kwa
kumaanisha, hatupaswi kuogopa kutekeleza yaliyo haki yetu.
Ndugu wanahabari
Kwa nafasi nitakayokuwa nayo
nitaanzisha semina, makongamano, mijadara itakayokuwa ya wazi na kutoa elimu ya
kutosha juu ya haki za wafanyakazi na wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi. Hii
itasaidia kupunguza migogoro na wafanyakazi watatambua haki zao.
Ndugu wanahabari
Tunatakiwa kuwa sauti ya
wafanyakazi hapa Tanzania, TUCTA imelala, tunataka kuikimbiza mchakamchaka,,
kuna mambo mengi yanatokea dhidi ya wafanyakazi hapa nchini lakini TUCTA haitoi
hata matamko au kutetea wafanyakazi,
Ndugu wanahabari
Natambua changamoto za
wafanyakazi, tunataka kuwa na
TUCTA Mpya
Nguvu Mpya
Uongozi Mpya
Sauti Mpya
Umoja Mpya
Maendeleo Mapya
Kwa pamoja tunaweza.
Mungu awabariki!
Dismas Lyassa
Mgombea nafasi ya Urais-TUCTA
simu 0754 49 89 72
HOTUBA
FUPI KUTOKA KWA JEBRA KAMBOLE, Wakili wa Dismas Lyassa anayefanya Kampuni ya
Uwakili ya Law Guards Advocates ya Jijini Dar-es-salaam kwa Waandishi wa
Habari.
Ndugu waandishi wa Habari wa vyombo vyote vya Habari,
Ndugu
watanzania wengine mliopo hapa,
Shukrani
Tunashukuru
sana kwa kuitikia wito wetu, Mungu awabariki sana, Tunamshukuru mwenyezi mungu
kwa kutupa afya na sia njema,
Ndugu waandishi wa Habari
Kuna
mambo muhimu manne tunataka kuwaeleza watanzania wote, hasa wafanyakazi na
viongozi wa vyama vyote vya wafanyakazi
Moja,
Ndugu anatimu iliyojipanga makini kuhakikisha TUCTA inarejea na kuwa na Nguvu
zaidi, Ni kijana makini mwenye malengo ya kuleta maendeleo ya haraka na kufufua
uhai wa TUCTA.
Ndugu Waandishi wa Habari
Napenda
kuchukua fursa hii kutoa onyo kwa wanaopanga kutoa rushwa kwenye huu uchaguzi
wa TUCTA kuwa tuko makini na hili tumejipanga, tutachukua hatua za haraka za
kisheria dhidi yao, ikiwa ni pamoja na kuwaripoti kwenye vyombo husika, Rushwa
si kipaumbele utapinga kwa nguvu zetu zote.
Ndugu Waandishi wa Habari
Ndugu
Dismas Lyasa pia atasaidia kuanzisha kituo au kushirikiana na mashirika mengine
kutoa masaada wa kisheria kwa wafanyakazi wanaofukuzwa makazini kinyume cha
sheria. Wafanyakazi wengi wakikumbwa na matatizo wafanyakazi wenzao
wanawatenga, vyama vyao vinawatenga, Dismas atahakikisha kuwa TUCTA ni kimbilio
lao.
Ndugu Waandishi wa Habari
Ndugu
Dismas Lyasa atasaidia kutoa mafunzo ya kisheria kwa wafanyakazi ili waweze
kutambua haki zao za msingi, kwa kuendesha semina, makongamano na mijadara
itakayotoa elimu na kuibua mijadara kwa wafanyakazi.
CHAGUA DISMAS LYASA KWA TUCTA MPYA, Mabadiliko ni
sasa,,,Asanteni


No comments:
Post a Comment