Habari za Punde

*GARI LA MAGEREZA LILIVYOSHAMBULIWA KWA RISASI NA MAJAMBAZI JIJINI DAR ES SALAAM JANA

MAJAMBAZI WALILISHAMBULIA KWA RISASI BASI LA JESHI LA MAGEREZA LIKIWA NA WATUHUMIWA NDANI LIKITOKA MAHAKAMA YA KAWE WAKIWAMO MAJAMBAZI SUGU NA KUJERUHI ASKARI WAWILI.

Habari za uhakika zimeifikia hivi punde kuwa tukio hilo limetokea muda mchache Jumatano Julai 2, 2014 eneo la Mikocheni karibu kabisa na hoteli ya Regency, wakati basi hilo likiwa njiani kutokea mahakama ya Kawe kurudisha watuhumiwa gerezani.
Askari magereza walifanikiwa kuondoka na watuhumiwa hao na haijafahamika mara moja hatima ya majambazi hao.
JINSI TUKIO HILO LILIVYOTOKEA
Shuhuda mmoja anasema kuwa, kuna gari ndogo ilikuwa inatokea njia ya Kawe kwenda Shoperz au ilikuwa inaelekea mjini kwa kutumia hii barabara ya Mwai Kibaki. 
''Hiyo gari ndogo ilipofika Maeneo ya Million Hairs Salon jirani kabisa na Regency park hotel ikakwama kwenye foleni ndefu sana, nyuma ya hiyo gari ndogo kulikuwa na magari mengine yameunga hiyo foleni.Gari ya magereza ikiwa na wafungwa ilikuwa ni kama ya sita au ya nne nyuma ya hiyo gari ndogo mara ghafla tukasikia puu puuu poo pooo kama risasi 6 au 8 hivi,kumbe ile gari ndogo inavyosemekana ilikuwa imebeba kiasi kikubwa cha pesa na hakukuwa na escort yoyote.
Majambazi wakiwa kwenye pikipiki waliifuata ile gari pale kwenye foleni wakamuamrisha yule jamaa atoe fedha na jamaa akaachia mkwanja. 
Sasa lile gari la magereza kwa vile liko juu sana kama gorofa askari wake wakaiona hiyo inshu live,sasa ile wanajiandaa tu na mabunduki yao' majambazi nayo wakashitukia mchezo na wakaanza wao kuwashambulia kwa risasi wale askari magereza.
Askari magereza ile wanajiandaa kujibu mapigo tu majambazi haooooo wakawasha pikipiki na kuondoka kwa speed kali.
'Kiukweli ilitisha na watu waoga kama mimi nilikimbia kujificha sehemu, yaani ilikuwa kama Movie''. anasimulia shuhuda huyo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.