Habari za Punde

*SAKATA LA WATANGAZAJI WA CLOUDS FM KUZICHAPA WAKIWA LIVE STUDIO 'NI UTOTO TUUUUU'

Kipindi maarufu kinachorushwa na Kituo cha Redio cha Clouds Fm, (XXL), jana kiingia dosali baada ya watangazaji wake Adam Mchomvu na Dj Fetty kuamua kuzichapa kavu kavu wakati wakiwa katika kipindi.

Katika hali isiyotegemewa na wengi watangazaji hao watatu maarufu kama, Dj Fetty, Adam Mchomvu na B12, waliamua kuweka Mic zao chini na kuanza kuzichapa bila kujali kuwa walikuwa wakisikilizwa na wasikilizaji lukuki kote nchini.

Tukio hilo lilitokea baada ya watangazaji hao kutokea kutoelewana  kuhusu mauzo ya Albam ya Fiesta. Na kama hukupata Fursa ya Kusikiliza >>BOFYA HAPA KUSIKIA<<

Walipotafutwa kwa njia ya simu, wahusika wa tukio hilo, Dj Fetty na B12 hawakutaka kabisa kuzungumzia suala hilo ili kujua chanzo cha kuanza 'KUTYSONIANA' ndani ya studio. 
PICHA YA STUDIO ZA CLOUDS BAADA YA TUKIO HILO LA KUZICHAPA

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.