Dar es Salaam Julai 11, 2014 Jamii zinazoishi katika Hifadhi Bioanuwai ya Milima
ya Usambara Mashariki zinatarajiwa kukuza uwezo wao wa kutumia rasilimali zao
za asili kwa njia endelevu. Kupitia mradi wa UNESCO wa Shilingi za Tanzania
milioni 700, “Uchumi wa Kijani katika Hifadhi Bioanuwai (GEBR) unaofadhiliwa na
KOICA (Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea), wananchi watapunguza
utegemezi wao wa kiuchumi kwa kukata miti. Mradi pia utasaidia kuchangia ulinzi
wa Hifadhi Bioanuwai ya Milima ya Usambara Mashariki (EUBR) na kupanua shughuli
za kiuchumi kwa ajili ya kupunguza umaskini na matumizi mazuri ya maliasili.
Baadhi ya shughuli za mradi huo kwa ajili ya kujenga uwezo zinahusisha
mafunzo ya aina tatu kwa jamii kuhusu Biashara ya Kijani katika Bioanuwai ya
Milima ya Usambara Mashariki huko Tanga. Mafunzo ya kwanza yanatarajiwa
kufanyika Julai 2014. Mafunzo hayo yataandaliwa na EUBR kwa kushirikiana na
Wizara ya Maliasili na Utalii. Jamii watapewa mafunzo juu ya mazingira ya
usimamizi wa biashara, masoko, uhasibu, fedha, ujasiriamali, na elimu ya
mazingira na viumbe hai. Jamii zitakazopata mafunzo zitaongeza uelewa wao juu
ya umuhimu wa kuunganisha masuala ya biashara na mazingira na kuanzisha akili
ya ujasiriamali ambayo itasababisha upanuzi wa biashara za kijani zilizopo na
kujenga nyingine mpya. Mafunzo mengine mawili yatafanyika mwishoni mwa mwaka
huu na mazingira tofauti, lakini ni kuhusiana na kuanzishwa kwa biashara ya
kijani.
Mjasiriamali wa biashara endelevu, Jason J Drew alisema ‘Hapo awali watu
waliongelea mikataba ya kibiashara inayoleta faida kwa pande zote mbili,
walikuwa wapuuzi, daima mazingira yalikuwa ndio yanayoshindwa. ' UNESCO inatumaini
kupitia mradi huu kwamba uasili wa kipekee, wa ajabu na wa kuvutia wa Tanzania
hautashindwa. Hata hivyo, katika mikutano ya kupanga na kushauriana iliyofanywa
na EUBR katika ngazi ya jamii Machi 2014, maoni ya pamoja yaliyowekwa kwa
muhtasari na wadau katika kuelekea kwenye biashara ya kijani ni 'Biashara ya
kijani kwa ajili ya kulinda viumbe hai ili kuongeza kipato bila kuharibu
mazingira'.
Karibu asilimia 38 ya ardhi ya Tanzania ni misitu na sehemu tambarare, na
ni pamoja na mazingira muhimu ya asili na makazi ya wanyamapori. Zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania wanaishi katika maeneo ya vijijini ambao
hutegemea sana maliasili na kilimo. Hali hii imekuwa kikwazo kwa
kuhifadhi misitu kutoka kwa shughuli za kiuchumi za binadamu .Ili kurekebisha
hali hii, Mpango wa UNESCO wa Binadamu na Bioanuwai (MAB) wa (1971) umekuwa ukiunganisha
binadamu na uasili badala ya kutenganisha viwili hivyo na miradi mbalimbali ya
ndani na nje ya hifadhi bioanuwai ambayo imesababisha maendeleo endelevu.
Nchini Tanzania, Hifadhi Bioanuwai ya Usambara
Mashariki mkoani Tanga iliteuliwa kama moja ya Hifadhi Bioanuwai mwaka 2000,
baada ya Hifadhi Bioanuwai nyingine mbili, Serengeti-Ngorongoro (1981) na Ziwa
Manyara (1981). Kanda ya Usambara Mashariki ni walengwa wa mradi wa GEBR, na unashughulikia
maeneo yanayozunguka wilaya za Muheza, Mkinga, na Korogwe.
Kutakuwepo na mafunzo kwa wananchi kuhusu bioanuai kuanzia tarehe 14 hadi
tarehe 24 huko Mkoani Tanga. Mafunzo ya
kwanza yatafanyika kijiji cha Mnyuzi, Tanga na waandishi wanakaribishwa
kuripoti.
Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
UNESCO Ofisi ya Dar es Salaam (dar-es-salaam@unesco.org)
P.O. Box 31473
127 C, Mtaa wa Mafinga (Kandokando ya Barabara ya Kinodoni)
Dar es Salaam Tanzania
Simu: +255-22-266 6623 Nukushi:
+255-22-266 6927. Mobile:Stella Vuzo 0767100 902


No comments:
Post a Comment