Makamu
Mkuu wa Misheni ya Uholanzi, Bi. Hinke Nanta (kushoto) akijadiliana jambo na
Katibu Mkuu Kiongozi (katikati) wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao
iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar
es Salaam.
Katibu
Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue akitoa nasaha zake kwa wanafunzi (watanzania)
waliopata udhamini kamili wa masomo nchini Uholanzi wakati wa hafla ya kuwaaga
wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la
Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Balozi
wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jaap Frederiks akitoa hotuba yake kwa
wanafunzi (watanzania) waliopata udhamini kamili wa masomo nchini Uholanzi
wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani
kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wanafunzi waliopata udhamini kamili wa masomo nchini Uholanzi wakisikiliza
kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue wakati
wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa
Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Wanafunzi
wakitanzania waliopata udhamini kamili wa masomo katika vyuo mbalimbali nchini
Uholanzi wakifurahi kwa pamoja wakiwa na wageni wegine waalikwa pamoja na mgeni
rasmi wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014
nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Benedict Liwenga-MAELEZO-DSM
**************************************************
Na Benedict Liwenga-MAELEZO
KATIBU Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue amehudhuria hafla
ya kuwaaga wanafunzi waliopata udhamini kwenda kusoma nchini Uholanzi katika
sekta mbalimbali zikiwemo za mafuta na gesi, miundombinu, kilimo, maji, afya
pamoja na Maendeleo ya sekta binafsi.
Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwa Balozi wa Uholanzi
eneo la Oysterbay Jijini Dar es salaam ambapo Katibu Kiongozi ndiye alikuwa
mgeni rasmi wa hafla hiyo.
Katibu Kiongozi amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa sana
wa program ilianzishwa na nchi ya Uholanzi wa kuwasaidia watanzania kupata
ufadhili kamili wa kwenda kusoma masomo mbalimbali nchini humo na ujuzi
wanaoupata uweze kulisaidia Taifa pamoja na watanzania wengine kwa ujumla.
“Ninaamini kuwa wanafunzi hawa waliopata ufadhili huu
wa masomo mbalimbali nchini Uholanzi watapata fursa kubwa ya kusomea mambo
mbalimbali na ujuzi huu hawatakaa nao wenyewe binafsi, bali watalisaidia taifa
na watanzania wengine, hivyo wajenge moyo huo wa kutokuwa wabinafsi”. Alisema
Sefue.
Naye Balozi wa Uholanzi
nchini Tanzania, Mhe. Jaap Frederiks amesema kuwa amefurahi kwa muamko mkubwa
wa watanzania wengi wa kuomba nafasi za masomo nchini kwake na amewaasa wengine
kuiga mfano huo kwani nchi yake itaendelea na programu hiyo kulingana na bajeti
pamoja na wataalam waliopo nchini Uholanzi.
“Nchi yangu inatoa fursa
ya masomo kwa watanzania kwenda kusoma lakini tunaangalia maeneo ambayo tuna
wataalam ambao wanaweza kuwasaidia watanzania kuwapa elimu, hivyo ni jukumu lao
wenyewe watanzania kuaamua maeneo gani ya kusomea pamoja na kozi wazipendezo”. Alisema Frederiks
Katika kipindi cha miaka Hamsini iliyopita, zaidi ya
watanzania Elfu tano wamepata udhamini wa kusoma katika sekta mbalimbali
zikiwemo Utawala wa Fedha, Uhandisi, Miundombinu, Kilimo, Afya, Elimu na
Utawala ambapo hii inaifanya Tanzania kuwa moja ya ya wanufaikaji wakubwa duniani
wa programu hii ya udhamini wa masomo, ambapo wengi wa watanzania waliopata
nafasi hizi wameshika nyazifa muhimu katika Jamii ya Tanzania kitu ambacho
kinaendeleza ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment